10/27/2010

Mikutano ya Kampeni Dar es salaam: JK amshitaki aliyemtusi

Na Mgaya Kingoba, Dar es salaam



MGOMBEA Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amemshitaki kwa wananchi mgombea ubunge wa Temeke kupitia Chadema aliyemtusi katika mkutano wa kampeni, akiwataka wamnyime kura yeye na chama hicho.

Amewafananisha mgombea huyo na chama chake kuwa majuha waliokata tamaa ndio maana wanatukana, na kuwataka wananchi wajihadhari nao kwa kuwanyima kura.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti akihutubia mikutano mikubwa ya kampeni Kiwalani Jimbo la Segerea na Kivule jimboni Ukonga mkoani Dar es Salaam.

“Vinywa vyao vichafu hujapata kuona. Nimeambiwa kwenye mkutano mmoja jana, sijui wapi (baadhi ya wananchi wakajibu Mwembeyanga) kuna mtu alikuwa akivurumisha matusi…mimi nilikuwa safarini.

“Wanazozana tu hao, ni mkusanyiko wa majuha, wameshakata tamaa. Jihadharini nao, dawa yao ni kuwashikisha adabu kwa kuwanyima kura,” alisema Rais Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi Kiwalani.

Akiwa katika mkutano wa kampeni jana kwenye Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, mgombea ubunge wa Chadema, Dickson Amos alitumia fursa aliyopewa na mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, kumtusi Rais Kikwete na mama yake.


Akiwa Kivule, alisema siasa ni malumbano ya sera kwa kuwashawishi wananchi namna utakavyoshinda.
 "

Katika mikutano yote hiyo, Rais Kikwete alifafanua Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2010 – 2015 kwa kueleza namna itakavyoshughulikia masuala mbalimbali nchini na katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika afya, alisema vituo vya afya vya Buguruni na Kivule vitapandishwa hadhi na kuwa Hospitali, na Hospitali ya Wilaya ya Amana itabaki kuwa ya Mkoa.

Alisema zahanati zote za kata zitapandishwa hadhi na kuwa vituo vya afya na vituo vya afya vitapandishwa kuwa hospitali ndogo ili zihudumie watu wengi kutokana na kata za Jiji kuwa na idadi kubwa ya wakazi.

Kuhusu Ukimwi, alisisitiza wananchi wa Dar es Salaam kujihadhari na ugonjwa huo hatari kwa sababu kasi ya maambukizi ni kubwa ikiwa ni asilimia 9.3 na watu 61,443 wanatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Akizungumzia maji, alieleza mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa kuboresha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu, Ruvu Chini na Mtoni.

Kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi, alieleza mikakati ya kuwapatia wafanyabiashara ndogo majengo kama la Machinga lililojengwa Uwanja wa Karume, Ilala, na pia kuendelea kutoa fedha kupitia mifuko mbalimbali.

Alisema katika Mkoa wa Dar es Salaam, vyama vya kuweka na kukopa vimeweza kutoa mikopo ya Sh bilioni 130.

Akiwa Kivule, alikubali ombi la mgombea ubunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa, la kutaka wakazi wa mji huo na ule wa Kipunguni kutohamishwa kwa madai eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya kujengwa viwanda.

“Nitawasaidia kulisemea hili katika mamlaka husika. Tutatafuta maeneo mengine ya viwanda, lakini hapa watu wataendelea kukaa, hilo limeishia hapo. Waambieni wawape vibali muishi,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na maelfu ya wakazi waliohudhuria mkutano huo.

Aliwanadi wagombea wa ubunge wa majimbo hayo, dk. Milton Mahanga na Mwaiposa, na kueleza kuwa wanatosha kushika nafasi hizo, hivyo kuomba wachaguliwe.

Mgombea huyo wa Urais wa CCM atakamilisha kampeni zake Jumamosi, siku moja kabla ya Watanzania kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa nne wa vyama vingi, huku akitabiriwa kupata ushindi.
…siyo kushindana kwa matusi jukwaani, kuchomana visu na kuua. Hawa hawaaminiki kushika madaraka ya nchi, ni sawa na kumpa fisi bucha kulinda,” alieleza Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema katika CCM, hawahubiri kumwaga damu, udini, kutukana wala mifarakano katika jamii kwa sababu mambo hayo hayapo katika sera za chama hicho.

Mkutano wa Kampeni Kata ya Kivule Jimbo la Ukonga: JK ahimiza amani na mshikamano, aahidi kuikabili kero ya maji Dar

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi akiwa na furaha na hamasa wakati anahutubia mkutano wa kampeni Jimbo la Ukonga leo. Mheshimiwa Kikwete aliwashukuru wana CCM kwa kuendeleza amani na utulivu kwani hata mikutano ya CCM ya kampeni ni ya furaha na kusheherekea mafanikio yaliyopatikana na kufafanua yale yanayo kuja.

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia kwa furaha hotuba ya mwenyekiti wa CCM taifa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo kwenye Jimbo la Ukonga. Mkutano huo ulitawaliwa na burudani na shangwe ambapo wana CCM walihimiza mshikamano na amani wakati wa mikutano ya kampeni.


Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo ameeleza kuwa serikali ya CCM ikipewa tena ridhaa ya kuongoza miaka mitano ijayo itahakikisha tatizo la maji jijini Dar es salaam linakwisha.

Mheshimiwa Kikwete aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni Kata ya Kivule jimbo jipya la Ukonga jijini Dar es salaam ambapo maelfu ya wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi kumsikiliza.

Alisema tatizo la maji Dar es salaam limekuwa sugu kwasababu nyingi zikiwemo
  • Uchache wa vyanzo vya maji ambavyo havitoshelezi mahitaji ya wakazi wa jiji
  • Mtandao wa maji uliopo sasa ni wa zamani na hivyo unahitaji ukarabati wa mara kwa mara
  • Maeneo mapya ya mji hakuna kabisa mtandao wa maji kutokana na ongezeko kubwa la watu Dar es salaam.
Alisema mahitaji ya maji kwa jiji la Dar es salaam kwa sasa ni mita za ujazo 360,000 na maji yaliyopo ni mita za ujazo 155,000 tu.

Aliongeza kuwa serikali ya CCM imeanza kushughulikia tatizo hilo ambapo utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa Kimbiji kuna maji mengi ya kutatua tatizo hilo. Baada ya uchimbaji wa visima kukamilika na mabomba kutandazwa, utafiti unaonyesha kuwa mita za ujazo 260,000 zitapatikana.

Mheshimiwa Kikwete pia alichukua muda mwingi kuelezea mafanikio yaliyopatikana miaka mitano iliyopita ikiwemo upanuzi mkubwa wa sekta ya elimu jimboni Ukonga. Alisema kuwa sasa hivi wanafunzi 42,120 wanaendelea na masomo ya sekondari ukilinganisha na miaka mitano iliyopita ambapo ni wanafunzi 10,000 tu waliokuwa wanaendelea na elimu ya sekondari.

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea, aliongelea mafanikio hayo (jimbo jipya la Ukonga) na kusema kuwa kati ya shule 34 za kata zilizojengwa hivi karibuni, 22 zimejengwa jimbo la Ukonga.

Kwenye mkutano huo pia walinadiwa wagombea udiwani na ubunge wa Jimbo la Ukonga ambapo wananchi walisema bado wanaimani na CCM na wana imani na Mheshimiwa Kikwete hivyo wataipigia kura CCM na wagombea wake. 

Mkutano wa Kampeni Kiwalani Jimbo la Ukonga (Segerea): Mahanga ajivunia shule za sekondari za kata


Wafuasi wa CCM, wakishangilia hotuba ya mgombea urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete, wakati alipohutubia mkutano wa kampeni huko Kiwalani nje kidogo ya jiji la Dar es salaam leo tarehe 27.10.2010.


Mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga (na sasa Segerea) Mheshimiwa Makongoro Mahanga amejivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye miaka mitano iliyopita ya upanuzi mkubwa wa elimu jimboni hapo.

Alisema ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010 imefanikisha ujenzi wa shule za sekondari 34 na kufanya jimbo hili kuongoza nchi nzima kwa ujenzi wa shule nyingi mpya nchi nzima.

Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni Kiwalani wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambapo leo yuko kwenye Mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya kunadi sera za CCM na kuomba wananchi ridhaa ya uongozi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, kabla ya kumkaribisha Mheshimiwa Kikwete kutoa hotuba yake ya kampeni, alichukua nafasi hiyo kuwasihi wananchi wa Kiwalani kuchagua CCM na wagombea wake. Pia alimuahidi Mheshimiwa Kikwete kwamba CCM mkoa watajitahidi ili CCM ishinde kwa kishindo, majimbo yote nane ya Mkoa wa Dar es salaam.

Kwenye hotuba yake ya kampeni Mheshimiwa Kikwete alisema CCM ni waaminifu na wakiahidi wanatekeleza ahadi zao hivyo wachague CCM iendelee kuongoza.

Aliongeza kuwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2005 - 2010, elimu ilipewa kipaumbele na kupewa asilimia ishirini ya bajeti ya serikali. Lengo la serikali ya CCM kutenga bajeti hiyo kubwa ni kukabiliana na changamoto zilizopo ili bajeti hiyo ikidhi mahitaji yaliyopo.

Akielezea mpango wa uboreshaji wa huduma ya afya, Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa mwaka 2005 CCM iliahidi Watanzania, itasogeza huduma za afya karibu na wananchi walipo na lengo ni kuwa Mtanzania asisafiri zaidi ya kilometa tano kufuata huduma ya afya. 

"Ndipo CCM ilipoanzisha mpango wa kujenga zahanati kwenye kila kata, na kwa kipindi cha miaka mitano inayokuja 2010 - 2015, zahati hizo zitapandishwa hadhi kuwa vituo vya afya, na kwa miji kama Dar es salaam, vituo hivyo vitakuwa hospitali ndogondogo". Alisema Mheshimiwa Kikwete. 

Mheshimiwa Kikwete pia alizungumzia mpango wa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo alisema jiji la Dar es salaam lina upungufu mkubwa wa maji kutokana na ongezeko la watu mijini.  

Kwa upande wa miundombinu ya barabara, Mheshimiwa Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanyika ili kukabiliana na changamoto iliyopo mijini kuwa na magari mengi kwa kufanya upanuzi wa barabara kubwa. "Lakini mpango mkubwa uliopo sasa ni wa kujenga barabara za juu "fly-overs" ambazo zitasaidia sana kupanga mji na pia kupunguza tatizo hili sugu. 

Mheshimiwa Kikwete pia alielezea jitihada mbalimbali za serikali yake kuwainua wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya fedha na uwezeshaji wa vijana kupata ajira. 

Mwishoni Mheshimiwa Kikwete alimnadi Dkt Makongoro Mahanga ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Segerea na madiwani wa kata zote jimboni hapo.  

10/26/2010

Mkutano wa Kampeni Nyamagana: Umati mkubwa wafurika kumsikiliza JK


Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa jimbo la Nyamagana alipowasili kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo.



Mapokezi makubwa yamemkaribisha Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza jioni hii.

Kwenye mkutano wake wa kampeni Mheshimiwa Kikwete alisema CCM ni chama kinachohubiri amani, utulivu na mshikamano na sio chuki na kupigana vita. Hivyo Watanzania wawape nafasi ya kuendelea kuongoza nchi kwa awamu nyingine tena. Alibeza vyama vya siasa vilivyoshindwa kuelezea sera zao na kuhubiri chuki au kutangaza vita.

"Siasa ni ushindani wa sera na mipango ya maendeleo na sio kushindana kurusha mawe na kutupiana matusi kwenye majukwaa" Alisema Mheshimiwa Kikwete huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wana Nyamagana waliofurika kwenye uwanja wa Sahara Kata ya Pamba, jimbo la Nyamagana.

Mheshimiwa Kikwete aliyetokea Chato mkoani Kagera, alielezea jitihada za CCM za kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kuboresha huduma za jamii. Alielezea mpango mkubwa wa kusaidia vijiji kumi na mbili vya wilaya hii ya Nyamagana kupata maji safi na salama, unaofadhiliwa na benki ya dunia.

"Miji na Vijiji kumi na nane vitapatiwa umeme katika mkoa huu wa Mwanza ikiwemo Nyamagana na Ukerewe" alieleza Mheshimiwa Kikwete wakati akielezea mpango mkubwa wa kuboresha huduma ya umeme.

Huduma nyingine alizozitolea ufafanuzi ni ile ya ujenzi wa barabara, kilimo kwanza ili kuendeleza wakulima na wafugaji, upanuzi mkubwa wa elimu n.k.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo mkubwa wa kampeni, mgombea ubunge wa Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Lawrence Kego Masha aliwahimiza wananchi hao kuwa makini na vyama ambavyo havitawaletea maendeleo na kuwasihi wachague CCM.

Mkuto wa Kampeni Nkome:JK apokelewa kwa Kishindo

- Maelfu wajitokeza kumlaki kwenye mkutano wa kampeni
-Amnadi Mgombea Ubunge Bwana Donald Max na Madiwani wote wa CCM


Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Bugando alipowasili kwenye mkutano wa kampeni Nkome Wilayani Geita leo.

Maelfu ya wananchi wa Nkome wakimshangilia mgombea urais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anahutubia mkutano mkubwa wa kampeni leo Nkome.

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi Nkome leo

Mapokezi ya aina yake yamefanyika hapa Nkome Tarafa ya Bugando wilayani Geita Mkoa wa Mwanza kumpokea Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi.

Mheshimiwa Kikwete amefanya mkutano mkubwa wa kampeni kata hiyo akinadi sera za chama chake akisisitiza mipango madhubuti ya CCM kwa miaka mitano ijayo ikiwemo ujenzi wa barabara na uimarishaji wa huduma za afya na maji.

Kabla ya hapo Mheshimiwa Kikwete pia alisimama vijiji vya Kasota na Nzera wilayani Geita ambapo pia alifanya mikutano ya kampeni na kunadi sera za CCM na kuwaombea kura wagombea udiwani na mgombea ubunge wa jimbo hilo.

Ikiwa ni siku yake ya mwisho ya kampeni mikoani, Mheshimiwa Kikwete anategemewa kufanya mikutano ya kampeni Muganza, Chato (Kagera), Nyang'wale na hatimaye Mwanza mjini kwenye uwanja wa Nyamagana.

10/25/2010

Mkutano wa Kampeni Sumve na Ngudu Wilayani Kwimba, Mwanza


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akipokea bendera ya CHADEMA, kutoka kwa mwenyekiti wa Wanawake wa chama hicho jimbo la Kwimba, Monika Jimotoli mara baada ya kutangaza kukihama chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jimboni humo. Monika amehama chama hicho na wenzake 18.


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akisalimia wananchi wakati akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni tarafa ya Nyamatala jimbo la Sunve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

- Mwenyekiti wa Chadema Kwimba atinga CCM na wengine 18: Asema CHADEMA Kwimba imekufa!- Kikwete aainisha malengo ya CCM kwa miaka mitano ijayo


- Awasihi wana Kwimba kuchagua tena CCM

Mheshimiwa Kikwete amewasihi wananchi wa Sumve leo kuchagua CCM kwani hakuna Chama kama CCM kwa ubora wa sera, utekelezaji wa sera na mipango na jitihada za kuleta maendeleo kwa watanzania.

Japo Tanzania bado ni nchi maskini, alieleza Tanzania ya mwaka 1961 na ya sasa sio sawa. “Lakini cha msingi ni kwamba yale tuliyoyaahidi tutayafanya, tumeyatekeleza” alieleza Mgombea Urais wa CCM, Mheshimiwa Kikwete kwenye mkutano huo wa kampeni.

Kwa upande wa elimu, Mheshimiwa Kikwete alisema serikali ya CCM imekabiliana na changamoto kuu nne zilizojitokeza baada ya upanuzi mkubwa wa elimu nchi nzima.

Changamoto zilizopatiwa ufumbuzi ni ile ya upungufu wa walimu ambapo kila kata kuanzia mwakani itapata walimu wa tano. Changamoto ya nyumba za walimu zitajengwa za kutosha kwa sababu bajeti ya elimu imeongezwa mara tatu zaidi kukabiliana na tatizo hilo. Na tatu ni changamoto ya vitabu vya sekondari ambapo Mheshimiwa Kikwete alieleza mipango imefanywa kushirikiana na Serikali ya Marekani ambapo wamesaidia kuchapisha vitabu vya sayansi vya sekondari. “Kwa hivyo kuanzia mwakani, watoto wetu wa masomo ya sayansi watakuwa na vitabu vya kutosha kwenye shule zote nchi nzima” alieleza Mheshimiwa Kikwete.

Kwa upande wa huduma ya afya, Mheshimiwa Kikwete alieleza mikakati ya serikali ya CCM kupambana na maradhi makubwa kama Malaria, UKIMWI na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake. Kwa kansa ya shingo ya uzazi, Mheshimiwa Kikwete alieleza kwamba kuanzia mwakani wanawake wote wenye umri wa kupata chanjo hiyo watachanjwa bure ili kukabiliana na gonjwa hilo sugu nchini.

Kwenye mikutano hiyo miwili pia Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa CCM iliahidi kuboresha utoaji huduma ya maji ili kufikia asilimia 60 vijijini na asilimia 90 mijini. Mheshimiwa Kikwete alieleza kwenye wilaya ya Kwimba, utoaji huduma ya maji kwa sasa umefikia asilimia 55.5, na bado jitihada madhubuti zinaendelea kuboresha hali hiyo.

Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa kwa msaada wa marafiki wa Tanzania wa maendeleo, vijiji kumi na mbili vya wilaya ya Kwimbavitapatiwa huduma ya maji kwenye mpango mkubwa wa usambazaji wa maji nchini unaodhaminiwa na benki ya dunia.

Kwa upande wa kilimo, Mheshimiwa Kikwete alielezea mpango mkubwa wa kilimo kwanza ambao unalenga kwenye kuboresha mambo makuu manane ambapo yatamsaidia mkulima kupata faida kwa kilimo chenye tija ikiwemo upatikanaji wa ruzuku na utafutaji masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.  

Mhehsimiwa Kikwete alieleza wakazi wa wilaya hii pia kwamba ilani ya CCM kwa mwaka 2010 – 2015 inaelekeza kipaumbele kwenye uvuvi wa samaki na kuendeleza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya wakulima.

Na kwenye mkutano wa kampeni huko Ngudu, aliyekuwa Mwenyekiti wa wanawake Chadema Wilayani Kwimba Mama Monica Jimotolo, amerudisha kadi ya chama hicho na kuingia rasmi CCM.

Mama Jimotolo alieleza sababu kuu iliyomfanya kuingia CCM ni kuchoshwa kwake na siasa za chuki na uchochezi ambazo zinalenga kuvunja amani na mshikamano wa nchi yetu.

Alieleza hadhara hiyo kuwa baada ya kufanya uamuzi huo, wengine kumi na saba wameongozana naye na kusema chama hicho kimekufa wilayani hapo. Wanachama hao walikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM taifa na kupewa kadi za Chama Cha Mapinduzi.  

Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge wa Chama Cha Mapinduzi. Aliwasihi wananchi wa Kwimba kupanga jozi iliyokamilika ya CCM ili kuleta maendeleo. Alitoa mfano wa kilimo cha punda na ng’ombe kwa kueleza kuwa unapoamua kulima utumie jozi ya punda au ya ng’ombe, lakini huwezi kuchanganya kwa kulima na ng’ombe na punda kwani punda atakapopiga mluzi, ng’ombe atasimama.

























10/24/2010

Kikwete aiteka Karatu, Maelfu wafurika mkutano wake wa kampeni sasa hivi







Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Karatu na vitongoji vyake wamefurika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo jioni hii.

Mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Karatu mjini ulifurika wana CCM na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumsikiliza Mheshimiwa Kikwete.





Umati huo kwa ujumla wake ulimueleza Mheshimiwa Kikwete kwamba wananchi wa Karatu wamechoshwa na sera za upinzani ambazo zimeshindwa kuleta maendeleo kwa miaka mingi.

Akiwauliza wananchi hao iwapo wako tayari kuipigia kura CCM na madiwani wake na mbunge, wananchi wao kwa ujumla wao wote walinyanyua mikono na kuonyesha ishara ya kuikubali CCM na kuwa wataipa kura zote.

Mkutano huo uliochangamka na uliokuwa na shamrashamra nyingi, ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumai ambaye aliwasalimu wananchi na kuwaomba wachague CCm kwa maendeleo ya kweli.

Mkutano huu ni wa mwisho kwa siku ya leo ambapo Mheshimiwa Kikwete alianzia Kibaya na Matui Mkoani Manyara. 

Baada ya Matui, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulielekea  Olkesumet na Mang'ola, kabla ya kuingia hapa Karatu mkoani Arusha.