6/22/2010

Jakaya Kikwete kachukua Fomu with STYLE













Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nd. Jakaya Mrisho Kikwete leo amechukua fomu ya kugombea tena urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi. Nataka niandike kwa kifupi jinsi mambo yalivyokuwa hapa Makao Makuu CCM kwani nahisi hotuba rasmi itatolewa na watu husika. Binafsi, nimependa style ya Jakaya aliyoingia nayo hapa. Akisindikizwa na familia yake, ameonekana mtanashati, na mwana CCM jasiri aliyeendesha Chama na Serikali kwa umakini hadi sasa.

Mgombea urais huyu ameingia hapa kavalia shati safi la linen ya kijani, suruali nyeusi na kiatu safi cheusi. Mi napenda vitu vya huyu mzee anavyovipangilia. Yaani mavazi yake. Ukiangalia harakaharaka hautaelewa, lakini kwa karibu nadhani hii ni Aldo shoe, very unique brand but very comfortable.

First lady yeye amevalia tenge la bazee la kijani na maneno ya njano yanayosomeka CCM na ile kanga ya begani nadhani ina picha ya mgombea. Na kama kawaida yake, juu kafunga kilemba, hii style ni very unique kwake na ina mpendeza sana. Siku moja nilimshawishi mke wangu afunge lakini akaniambia hatoweza kufunga kama la Mama Salma Kikwete.

Watoto wote wamefika pia. Ridhiwani yeye kavalia shati lake la kijani lakini wengine wote wamevaa T- Shirts 2010 KIKWETE. Hizi zinavutia sana zipo za kijani, njano na nyeupe. Inaonyesha jinsi familia hii ilivyokuwa na mshikamano, na wanavutia kweli kweli.

Kwa maneno yake mwenyewe amesema awamu hii ya pili itakuwa ya
Ari zaidi,
Nguvu zaidi,
Kasi zaidi,
Kwa Pamoja tutaweza kuleta Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania.

Kimsingi mimi nilivyomsoma mgombea ni kwamba hii ya sasa ni muendelezo wa ile kampeni yake ya kwanza aliyoahidi Maisha Bora Kwa kila Mtanzania Kwa Nguvu Mpya, Ari Mpya na Kasi Mpya. Jamani mgombea yuko makini maana hii inaonyesha ya kwamba zoezi la kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania liko pale pale, ila kwa sasa lina Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

Mambo matatu yaliyomshawishi kuchukua fomu kwanza kabisa kukubali ushawishi wa wana CCM wenzake waliomsihi kuendelea na kipindi chake cha pili cha uongozi kutokana na imani kubwa wananchi na wana CCM waliyokuwa nayo kwake. aliyowaonyesha wana CCM na Watanzania kwa ujumla.

Pili yeye mwenyewe ameridhika na uongozi wake na ule wa serikali yake ya awamu ya nne kwa ujumla. Hakuna bahari isiyokuwa na mawaimbi. Hivyo hata yeye mgombea kwa kipindi chake cha kwanza amepita bahari yenye mawismbi na misukosuko mingi lakini ameweza kuvuka salama na kuwavusha salama Watanzania wote.

Tatu, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamruhusu kufanya huivyo.kwa sababu hizi kuu tatu, mgombea urais ameamua kuchukua fomu leo kwa awamu nyingine ya pili ya uongozi wa juu kabisa nchini Tanzania.