10/10/2010

Mkutano wa Kampeni Songea Mjini katika Picha

Hivi ndivyo meza kuu ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ilivyopambwa kwenye uwanja wa Majimaji Songea Mjini leo.

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM mheshimiwa Jakaya Kikwete akimtambulisha mgombea Ubunge wa jimbo la Songea Mjini kupitia chama hicho ndugu Emmanuel Nchimbi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Songea

Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi akiingia kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea huku akipungia na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliofurika katika uwanja huo katika siku yake ya kwanza ya kampeni katika mkoa wa Ruvuma tarehe 10.10.2010.

Umati wa wana Songea Mjini wakimsubiri Mheshimiwa Kikwete

Mara tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa mjini Songea tarehe 10.10.2010 kwa ajili ya kufanya kampeni katika mkoa wa Ruvuma, Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwasalimia chipukizi waliofika uwanjani kwa lengo la kumpokea.

Mgombea Urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Kikwete anaangalia ngoma ya asili iitwayo beta inayochezwa na wananchi wa kabila la wangoni ambao hutumia mianzi (mbeta) iliyochanwa nyufa ndogondogo huku kijiti kikitumika katika kupiga mwanzi huo wakati wa kumkaribisha mara tu alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa Songea

Umati ukimshangilia Mheshimiwa Kikwete akiingia uwanjani


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mzee Mustapher Songambele,pamoja na Paul Kimiti kwa pamoja wakicheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na msanii wa kizazi kipya ajulikakaye kwa jina la Maloo mara baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni kwenye uwanja wa Majimaji huko Songea


Wapanda pikipiki wakisindikiza msafara wa JK alipokuwa anaingia uwanja wa Majimaji Songea Mjini leo.

No comments:

Post a Comment