7/10/2010

Breaking News - Mrema katikati ya wana CCM akiimba shangilia ushindi unakuja


Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakimzingira Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema wakati alipotumi nafasi ya kutoa salamu za chama chake kwa kumwagia sifa tele Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutekeleza kwa ufanisi program mbalimbali za maendeleo nchini, pia alisifia sana uimara wa chama cha CCM na nidhamu ya chama.

Uzuri wa ndege manyoyaaaaa

Uzuri wa CCM seraaaaa

Huu ni ujumbe wa Khadija Kopa akimfagilia Mheshimiwa Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa Chama Cha TLP alipofungua moyo wake akimmwagia sifa kede kede Mwenyekiti wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete.Hapa sasa hivi Lyatonga Mrema anatoa salamu rasmi kutoka chama cha TLP na kuwasema wale wanaosingizia katumwa na wana CCM wakome.

Anashangiliwa na wana CCM kwa nyimbo na vigelegele, anasema kwamba CCM haikamatiki. CCM Chama Kubwa, amesalimu amri. Kwani mwaka 1995 alishindwa, mwaka 2000 aligaragazwa na Mh. Mkapa, na mwaka 2005 ndio kabisaa Kikwete akammaliza. Hivyo CCM ni chama imara, hakishikiki. "Kweli CCM inagaragaza upinzani".Mheshimiwa Mrema aliongeza, "Kila mwaka wa uchaguzi inakula kwangu, sasa nimechoka" anasema Mrema kwa hamasa huku akiendelea kusifia CCM na uongozi wake.Kwa maneno yake amesema, hana sababu ya kuacha kumsifia Rais Kikwete kwani ndiye Rais pekee anayemjua. Amefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka mitano hususan katika harakati za kupambana na ufisadi na mafisadi nchini.Amekiri ya kuwa katika marais wengi waliopita, Kikwete ni mthubutu na mtekelezaji. Anaumia roho sana kusikia kuna watu wanaombeza ati hajafanya lolote hivyo wamtose.Mrema amewasuta wote wanaobeza maendeleo ya serikali ya Rais Kikwete na amewaomba wana CCM waendelee kumsaidia ili afanye vizuri zaidi. Hapo Mrema alishangiliwa sana kwa nyimbo za CCM na kusindikizwa na bendi ya TOT.


Mrema amemaliza kwa kusema ya kwamba anafuata wosia wa baba wa Taifa na hivyo atagombea ubunge vunjo kupitia chama chake cha TLP.


Mwenyekiti wa CCM amemshukuru kwa kuwa mkweli lakini amemuhakikishia ya kwamba hata wana CCM watakwenda huko VUNJO na watakutana tena.


Mambo moto moto hapa Kizota, salamu zinaendelea. Picha zinakuja

2 comments:

  1. Yaani Lyatonga ametoa mpya. CCM ni jukwa tosha la kutangaza nia ya kugombea ubunge Vunjo... hahaha.. Duh!By the way Mkutano Mkuu huu wa Chama inapendeza na maandalizi yamekamilika kikamilifu. Hongera sana. Very very impressive.

    ReplyDelete
  2. Nahitaji ku support ccm kwenye kampen zote hasa kutangaza au kupigia debe kupitia my blog www.musoma-tanzania.blogspot kama kuna chochote basi email to me .

    ReplyDelete