7/01/2010

Jakaya Mrisho Kikwete arudisha Fomu za CCM Leo Dodoma


Leo tarehe 01 Julai, 2010 Nd. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kurudisha fomu za kuwania Urais kwa awamu ya pili kupitia Chama Cha Mapinduzi. Zoezi hili litarushwa live na ITV na kwa wale walio nje ya Tanzania wataweza kuangalia kupitia mtandao wa internet. Link inapatika kwenye website ya CCM. www.ccmtz.org. Muda wowote kuanzia sasa Mwenyekiti wa CCM atafika hapa. Habari zaidi zinakuja.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiingia makao Makuu ya CCM leo kurudisha fomu ndani ya chama hicho kwa ajili ya kugombea urais.

Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiingia Makao Makuu CCM akisindikizwa na Mheshimisa Chiligati na Msaidizi wa Rais - Siasa Bwana Rajabu Luhwavi.

Umati wa wana CCM wakiimba kwa shangwe kumkaribisha Mwenyekiti wao Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipoingia Makao Makuu ya CCM leo.

Kikundi cha Ngoma ya asili ya Wagogo waliopo mjini Dodoma nao wakitumbuiza kwa hamasa kubwa wakati Mwenyekiti wa CCM alipoingia kurudisha fomu leo.

Baadhi ya mafundi mitambo wakiwa wanahakikisha tukio hili linaonekana na watanzania wote ndani na nje ya nchi yetu. Pichani ni Salum Mkambala wa ITV ambao walirusha matangazo hayo live, akiwa pamoja na Prof. Ngalinda yeye ni IT specialist wa CCM.


Baadhi ya wanavyuo wa vyuo vikuu wakiwa na bango rasmi kumshukuru Rais Kikwete kwa kuendeleza elimu ya juu nchini. Baadhi ya hawa wanavyuo sio wana CCM lakini wamejumuika na wenzao kutoa asante kwa Mheshimiwa Rais.

Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Beno Malisa na Ridhiwani Kikwete mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM wakikamilisha maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti wa CCM wakati anarudisha fomu. Vijana hawa wawili ndio waliosimamia zoezi zima la kuzuka Tanzania nzima kutafuta udhamini kwa Mh. Rais Kikwete kwa ajili ya kugombea tena Urais. Rais Kikwete amewashukuru vijana hawa kipekee kwa niaba ya wenzao wote waliozunguka kanda nane Tanzania kuomba wadhamini.

No comments:

Post a Comment