7/11/2010

Salamu za Dr. Shein kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM

Safu ya viongozi wa CCM wakisikiliza mkutano unaoendelea Dodoma

Dr. Shein amewashukuru wana CCM wote kwa imani waliokuwa nayo kwake na ameahidi kuipeperusha bendera ya CCM barabara katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea urais kupitia tiketi ya CCM.

Baadhi ya mambo aliyoyaainisha kwa wajumbe kama mgombea urais Zanzibar ni:

- Kuendeleza na kudumisha mapinduzi visiwani Zanzibar

- Kuimarisha muungano na kumaliza kabisa changamoto za muungano

- Kusimamia suala la amani na utulivu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Watanzania wana kila sababu ya kushikamana na kujivunia amani na mshikamano ndani ya nchi yetu.

- Kuendeleza jitihada za Rais Abeid Aman Karume visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo. Hivyo ataweka utaratibu wa kuenzi na kuendeleza yale mazuri ya kimaendeleo aliyoyafanya Rais Karume.

Aidha Dr. Shein ametoa shukrani zake za dhati kwa Dr. Salmin Amour rais mstaafu wa Zanzibar ambaye alimteua Dr. Shein kwa mara ya kwanza kuingia kwenye baraza la wawakilishi.

Shukurani nyingine amezitoa kwa Mheshimiwa Rais Karume aliyemteua kuwa Naibu Waziri wa Afya na baadae Waziri wa Katiba na Sheria. Amemshukuru Rais Msaafu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa aliyemteua kuwa Makamu wa Rais baada ya Makamu wa Rais wa wakati huo hayati Dr. Omar Ali Juma kutangulia mbele ya haki.

Mwisho Dr. Shein aliwashukuru viongozi wengine wote walioshirikiana nae katika kipindi chote alichoongoza kama Makamu wa Rais na ngazi nyingine mbalimbali za uongozi alizopitia bara na visiwani. Pia Dr. Shein ameshukuru familia yake na mke wake Mama Mwanamema Shein kwa kuwa msaidizi wake wa karibu na kumsaidia kuwa kiongozi mzuri hadi sasa kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM visiwani kwa nafasi ya urais.

Dr. Shein ameahidi kufanya kampeni safi visiwani, pindi muda utakapowadia. Atafafanua sera za CCM na anaimani ushindi utapatikana kwani CCM lazima iendelee kuongoza.

No comments:

Post a Comment