Karibuni kwenye blogspot Jakaya Kikwete 2010. Blogspot hii ina habari za siku 70 za Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete. Blog hii haitakuwa na habari baada ya tarehe 30 Oktoba, 2010
7/12/2010
Dr. Bilal amshukuru Mwenyekiti wake, aahidi ushindi wa KISHINDO
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dr. Gharib Bilal kama Mgombea Mwenza kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa Tanzania mwezi Oktoba.
Mmoja wa wakereketwa wa CCM Mkoani Dodoma akiimba CCM Chama wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili kwenye uwanja wa Michezo wa Jamhuri mjini Dodoma.
Baadhi ya vijana wa CCM waliokuwa wamevalia Tshirts maalum za vijana wa mkoa wa Dodoma zilizoandikwa KIKWETE 2010. Vijana hawa walihamasisha umati kwa nyimbo zao na furaha waliyokuwa nayo wakati viongozi wa Chama wakitambulishwa.
No comments:
Post a Comment