7/11/2010

Mkutano Mkuu wampitisha Jakaya Kikwete kwa KISHINDO

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya silimia 99 kuwa mgombea pekee wa Urais kwa tiketi ya CCM(picha na Freddy Maro)
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya mrisho Kikwete akiondoka kwenye meza kuu kabla ya wajumbe kupiga kura kumchagua kuwa mgombea wa urais kupitia CCM
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekezwa mahali pa kukaa pamoja na wajumbe wengine wa Mkutano Mkuu ili kuruhusu upigaji kura uendelee.
Majibu yametoka na Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa na kupitishwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama Cha Mapinduzi kama Mgombea wa Urais kupitia chama chake cha CCM.

Wapiga kura walikuwa 1909, hakuna kura iliyoharibika.
Kura za Ndio 1893 ambazo ni sawa na asilimia 99.16.

Kura za Hapana 16 ambazo ni sawa na asilimia 0.84.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tisa wanampongeza kwa nyimbo za ushindi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments:

Post a Comment