7/10/2010

Burudani ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM - Kizota, Dodoma

Dokii a.k.a suprise aliimba na kucheza kwa madaha akishukuru CCM kwa kuwapa nafasi vijana kupata nafasi katika chama. Style ya nywele ya Dokii iliwapendeza wengi kwani ilikuwa na rangi za bendera ya taifa - bluu, njano, nyeusi, njano na kijani.
Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili Flora Mbasha na kundi lake zima waliinua mashabiki wengi wa nyimbo za injili na wimbo wao uliokuwa na speed ya kasi na uliowasisimua wengi. Wimbo huo ulisifu uongozi wa Mwenyekiti wa CCM ukisihi kuongeza ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kuleta maendeleo Tanzania.

Kada wa CCM mwanadada Vicky Kamata akitumbumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu na wimbo wake mpya kuhusu uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete.

Wasomaji utenzi kutoka Tanzania visiwani walitunzwa na kuinua wajumbe wengi vitini kwa mpangilio mzuri wa mashairi yao yaliyoisifu nchi ya Tanzania na viongozi wake mahiri.

Baadhi ya vikundi vinavyotumbuiza leo ni Vijana wa CCM Vyuo Vikuu, Tanzania One TOT, Wanaume TMK, Flora Mbasha, Vicky Kamata, na wengine wengi.

Lakini waliofunika na kushangiliwa na umati wa wajumbe wengi ni vijana wa CCM wa vyuo vikuu kwa ujembe wao uliokuwa na vijembe kebekebe kwa wapinzani.

Video clip ya wimbo huu itapanda hewani pindi internet itakapostabilize. Lakini baadhi ya maneno kwenye wimbo wao ni kwamba mikoa yote waliyopita kutafuta udhamini wananchi walisema chaguo lao ni Jakaya Kikwete na CCM. Wanamuasa Jakaya asiwe na hofu hao wapinzani ni kama "mavuvuzela" hayatamzuia kufunga goli la ushindi.

No comments:

Post a Comment