Karibuni kwenye blogspot Jakaya Kikwete 2010. Blogspot hii ina habari za siku 70 za Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete. Blog hii haitakuwa na habari baada ya tarehe 30 Oktoba, 2010
7/10/2010
Mkutano Mkuu katika Picha Kizota, Dodoma Leo
Captain George Mkuchika akihamasisha wajumbe kabla ya hotuba ya Mwenyekiti wa CCM ya kuwakaribisha wajumbe kwenye Mkutano Mkuu. Mwakilishi wa Matawi ya CCM nje ya nchi akitoa salamu kwa niaba ya wanachama wa CCM nchi mbalimbali ambao baadhi yao wamekuja kuhudhuria mkutano mkuu.
Baada ya salamu zao Mheshimiwa Chiligati alieleza wajumbe ya kwamba wanafanya mazungumzo na Vyama Vya Upinzani ili kuruhusu watanzania waliopo nje ya nchi kuweza kupiga kura wakati wa chaguzi kuu nchini Tanzania.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakiimba na kushangilia wimbo maalum uliotungwa na kuimbwa kwa umahiri na vijana wa CCM walio kwenye Vyuo Vikuu. Baadhi ya maneno yaliyowakuna wengi ni "wapinzani tuwachape kwa kura ya ndio, Kikwete Kiboko yao, usiogope kelele za mavuvuzela, ushindi lazima"
Mwneyekiti wa UWT Taifa Mama Sophia Simba akishangilia burudani ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment