7/12/2010

CCM Diaspora wamsalimia Mwenyekiti wa CCM Ikulu Dodoma

Bi Susan Mzee akisoma ripoti ya maendeleo kutoka Tawi la CCM -Uingereza ambalo lina miradi mbalimbali ya maendeleo.



Bi Zainab Janguo akitoa salamu kutoka CCM tawi la Marekani wakati wana CCM waishio nje ya Tanzania walipofika Ikulu Dodoma kumsalimu na kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambnaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea wa Urais kupitia CCM.




Mwakilishi wa CCM Tawi la Uingereza Susan Mzee ametoa taarifa fupi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu Dodoma kuhusu maendeleo ya Matawi Ya CCM nje ya Tanzania.
Wana CCM wanaoishi nje ya nchi wameleta salamu hizi Ikulu wakisindikizwa na Waziri Wa Mambo ya Nchi za Nje Mheshimiwa Bernad Membe, kwa mualiko wa CCM. Wanachama hawa wako nchini kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tisa wa Chama Cha Mapinduzi ulioisha jana mjini Dodoma. Wanachama hawa wametokea nchini Uingereza, Marekani, Italia, Uganda na India.
Salamu walizokuja nazo ni pamoja na pongezi na shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa uongozi wake kwenye CCM na kutambua mchango wa matawi ya CCM nje ya Tanzania.
Aidha waliwapongeza waasisi wa matawi haya walioshawishi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 2002 kuandikisha wanachama wa CCM nje ya Tanzania. Waasisi hao ni Hayati Mheshimiwa Amina Chifupa na Nape Mnauye.
Mojawapo ya maombi waliyoainisha kwa Mwenyekiti wa CCM ni kuwapatia mafunzo kwa makada wa CCM ili waweze kuendeleza Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza kwa jitihada zao, na kuwasihi wasisahau kuleta maendeleo nyumbani. Ameahidi kusaidia yale mambo ambayo yatakuwa ndani ya uwezo wake na mengine atamuomba Mheshimiwa Membe asaidie.

No comments:

Post a Comment