7/13/2010

Wanamziki wa Kizazi Kipya Wakutana na Rais Kikwete, Ikulu Dodoma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ruge Mutahaba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, walipomtembelea Ikulu, Dodoma leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msanii aliyeimba wimbo maarufu unaopendwa na wengi "pipi" Marlow, alipokutana na wasanii Ikulu, Dodoma.

"Kazi nzuri" Hivi ndivyo Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alivyosikika akimwambia msanii huyu mwenye kipaji cha kucheza muziki wa kizazi kipya. Msanii huyu anatokea taasisi ya kuibua vipaji ya THT.


Mwanamuziki chipukizi Lina Sanga akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Dodoma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msanii kutoka TMK "Mheshimiwa " Temba ambaye wakati akijitambulisha kwa Rais alimfurahisha kwa kusema "Mheshimiwa Rais, Mimi naitwa Mheshimiwa Temba"


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Msanii wa kizazi kipya maarufu kama C - P


Baadhi ya wasanii wakipata chakula cha mchana kwa mualiko wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Dodoma leo mchana.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia baadhi ya wasanii waliofika Ikulu Dodoma leo kwa mualiko wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwanafalsafa au Mwana FA akitoa salamu zale kwa Rais na kwa wanasanii wenzake waliolikwa Ikulu Dodoma leo.


Lina Sanga maarufu kama Lina ambaye ni product ya Tanzania House of Talent, taasisi ambayo inaibua vipaji na waimbaji nchini Tanzania. Wimbo wake mashuhuri alioutoa hivi karibuni na Barnaba ni Wrong Number.

Mchezaji Kiduku mashuhuri Athumani akimsalimia Rais Jakaya Kikwete na kumshukuru kwa kutambua vipaji vya vijana wa Kitanzania katika fani ya muziki na hata wachezaji.
Athumani pia ameibuliwa na Tanzania House of Talent.

No comments:

Post a Comment