7/18/2010

Mwenyekiti wa CCM Taifa Apokelewa Dar kwa kishindo, awatambulisha wagombea Mnazi Mmoja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Dar es salaam na Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, kwa ajili ya kumtambulisha mgombea huyo pamoja na Mgombea Urais wa Zanziabar kwa Tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanziba kwa tiketi ya CCM Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakiagana na wananchi wa Kisiwa cha Pemba katika Uwanja wa Ndege wa Karume leo, baada ya kukamilisha ziara yao ya siku mbili kisiwani humo ambapo jana Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume aliwatambulisha Wagombea hao kwa Wananchi wa Kisiwa hicho katika uwanja wa Gombani ya kale Chakechake Pemba.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege wa kmataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mara tu alipowalisili akitokea mjini Dodma ambapo alilihutubia Bunge

No comments:

Post a Comment