7/11/2010

Mwenyekiti wa CCM amtambulisha Dr. Shein

Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtambulisha rasmi Dr. Ali Mohamed Shein kama mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti amemuelezea Dr. Shein kama kiongozi mzoefu, jasiri, imara na anafaa kupeperusha bendera ya CCM visiwani Zanzibar. Mwenyekiti alieleza Halmashauri Kuu ya CCM ilimpitisha kwa kura za kutosha, na wana CCM wote wanaheshimu uchaguzi huo.
Mwenyekiti alieleza kwamba kulikuwa na wagombea 11 na wote walikuwa wanagombea nafasi moja, japo wote wanafaa na wote wazuri, lakini hakukuwa na namna ya kuwapitisha wote. Ilibidi achaguliwe kiongozi mmoja. Na kiongozi aliyechaguliwa ni Dr. Shein, wagombea wengine wanaombwa wamuunge mkono Dr. Shein ili kazi ya kujenga taifa iendelee.

No comments:

Post a Comment