8/02/2010

Breaking News.....mwingine wa Chadema a-cross over kwenye Neema CCM

Livinus Mashindano akisalimiana na wanachama wa CCM mara baada ya kushuka jukwaani kutangaza kuwa ameingia CCM. Mashindano alikabidhi kadi nyingine nne za wanachama vijana wa Chadema walioingia naye CCM.Livinus Mashindano ameingia rasmi CCM kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Mashindano ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es salaam na alikuwa Katibu wa Chadema wilaya ya Ilala.

Mashindano amekabidhi kadi nyingine nne (pamoja na yake) za vijana wa Chadema ambao wameamua kwa ridhaa yao wenyewe kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Mashindano alisema anajisikia vizuri sana kuingia CCM na anaamini kuwa atashirikiana na vijana wengine wa CCM ili kuendeleza CCM. Alikiri ya kuwa japo ni mara yake ya Kwanza kusema maneno "CCM JUU" lakini alikuwa na furaha na mapokezi ya wana CCM.

Baada ya Mashindano kuthibisha kwa maneno yake mwenyewe kwamba anajiunga rasmi na CCM bila ya kulazimishwa, Mashindano alivalishwa kofia ya CCM, shati la kijani na alililakiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments:

Post a Comment