8/26/2010

Mkutano wa Kampeni Ngara, Kagera - JK Majibu ya Sekondari yanapotoka ni vicheko Kila Nyumba

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wananchi wa Ngara leo kwamba jitihada zao za kujenga shule za sekondari za kata zimezaa matunda.

Pindi majibu ya waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza yanapotoka, vicheko hutawala kila nyumba kwani ufaulu umewiana na idadi ya watoto wanaoingia kidato cha kwanza.



Mheshimiwa Kikwete alisema kwenye Wilaya ya Ngara peke yake mwaka 2005, wanafunzi 480 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. Mwaka 2010 wanafunzi 3840 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. Haya ni mabadiliko makubwa kwenye upande wa elimu, Mheshimiwa Kikwete alisema. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za CCM.

Mafanikio mengine aliyoyazungumzia ni upanuzi na ujenzi wa barabara mpya kwenye mkoa wa Kagera, upatikanaji wa umeme, maji safi na salama ma muendelezo wa sera za kilimo kwanza. Hii yote ni kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanapatikana.

Alihimiza wananchi wafanye jitihada kufuatilia utendaji kazi wa halmashauri zao ili kujua fedha walizotengewa zinatumika ipasavyo kuendeleza halmashauri zao.

Msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulianza siku ya sita ya kampeni kwa kufanya mkutano wa kampeni mjini Ngara, Rulenge, Nyakahura, Lusahunga, Biharamulo, Kakonko, na baadae kulala Kibondo.

No comments:

Post a Comment