8/23/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo Mkoani Mwanza

Kampeni ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutafuta nafasi ya kuongoza tena nchi, imeingia katika siku yake ya tatu leo.
Shamrashamra ya msafara wa Rais Kikwete ulianzia Ikulu mjini Mwanza na kuvuka kivuko kuelekea Buchosa, Sengerema. Msafara wa Rais Kikwete umepambwa na Mbunge wa Serengerema ambaye hana mpinzani Mh. Ngereja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Kandoro.
Baada tu ya kuvuka kivuko Mheshimiwa Rais alisimama Kamanga (kivukoni) kuzungumza na umati wa watu waliokuwa wakimsubiri.
Aliwasalimu na kuwaomba wamchague tena kama mgombea Urais kupitia CCM pamoja na wabunge na madiwani wa CCM ili kazi aliyoianza iendelee.
Mheshimiwa Kikwete pia alisimama na kuzungumza na wananchi wa Katunguru, Kasenyi, Luchili, Busumba na hatimaye aliingia Buchosa ambapo ndipo siku ya tatu ya kampeni zake inaanzia hapo.

No comments:

Post a Comment