8/31/2010

Mkutano wa Kampeni Mbeya Mjini: JK anasimikwa na Wazee wa Mbeya, akabidhiwa vifaa Vya KaziChifu Mkuu wa Mbeya Chifu Mweshenga na machifu wengine wa wilaya zote Mkoani Mbeya wamemsimika Mheshimiwa Jakaya Kikwete ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Mkoa wa Mbeya na alama ya uongozi.

Wakimsimika rasmi kama kiongozi, machifu hao wamesema ujio wa wana CCM na wananchi wengi Mkoani Mbeya ni ishara nzuri ya ushindi wa kishindo kwa CCM na Mheshimiwa Kikwete.
Chifu Mweshenga ameanza kwa kumvika shuka nyeupe ishara ya uongozi wa ki-chifu kwa mkoa wa Mbeya. Pia Chifu huyo amemkabidhi Mheshimiwa Kikwete Mkuki na kusema "Mheshimiwa wewe ni kiongozi sasa lakini pia ni mwanaume (hivyo kwa mila yetu) unatakiwa kuwa na mkuki nyumbani"

Mwisho kabisa machifu hao wa Mkoa wa Mbeya walimkabidhi Mheshimiwa Kikwete kiti cha jadi na kusema kwamba wao wanaamini kuwa mgombea huyu wa CCM atarudi Ikulu, na hivyo atumie kiti hicho kukalia na kufanya maamuzi muhimu ya uongozi.

Ujumbe huu wa Machifu uliongozwa na Chifu Mkuu Mkoani Mbeya Chifu Mweshenga, Katibu wa Machifu Mkoa Chifu Mwaluego, Chifu Kiongozi Mkoa Chifu Lioto, Chifu Mwongole na Chifu Richard Mwavipa.

No comments:

Post a Comment