8/23/2010

Kampeni katika Picha: Buchosa - Sengerema - Geita

Rais Jakaya Kikwete akiaagana kwa kuwapungia mkono maelfu ya wananchi wa mji wa Geita mara baada ya rais kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni tarehe 23.8.2010.
PICHA NA JOHN LUKUWI
Wananchi wa mji wa Geita wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao ili wamchague katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 31.10.2010.Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwahutubia maelfu ya wananchi wa mji wa Geita katika siku yake ya pili akiwa mkoani Mwanza tarehe 23.8.2010.


Rais Kikwete akiwa amesismama kwenye gari yake akiwapungia wananchi wa Nyehunge wenye shauku ya kumsalimia Rais Kikwete mara baada ya kuwahutubia tarehe 23.8.2010Rais Kikwete akiongea na msichana albino katika kijiji cha Nyehunge mara baada ya kumaliza kuwahutuia mamia ya wananchi wa kijiji hicho.Mamia ya wananchi wa kijiji cha Nyehunge katika jimbo la Buchosa waliojitokeza kumsikiiza rais Jakaya Kikwete alipowatembelea na kuomba wampigie kura katika uchaguzi mkuu ujao.


No comments:

Post a Comment