8/22/2010

Rais Jakaya Kikwete awasili jijini Mwanza, ahutubia maelfu Kirumba, awaondoa shaka wa Misungwi

Rais Kikwete akisalimiana na Mh. Masha (Nyamagana) na Mh. Ngereja (Sengerema) ambao wote hawana upinzani kwenye majimbo yao kutoka mkoa huu wa Mwanza.
Mgombea akikagua gwaride la chipukizi mara baada ya kuwasili mjini Mwanza tayari kuanza siku ya pili ya kampeni zake za Urais kupitia tiketi ya CCM.

Baadhi ya wagombea ubunge kanda ya Ziwa wakimsubiri Rais Kikwete mgombea urais tiketi ya CCM kabla ya kutua uwanja wa ndege Mwanza leo.


Wageni mbalimbali waliofika kiwanjani kumlaki mgombea urais wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika siku yake ya pili ya kampeni ya kurudi tena kuongoza nchi.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia maelfu ya wananchi wa jiji la Mwanza waliofurika katika uwanja wa CCM Kirumba katika siku ya kwanza ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi katika mkoa huo tarehe 22.8.2010

No comments:

Post a Comment