8/26/2010

Mkutano wa Kampeni – Rulenga: JK Akabidhiwa Silaha za Jadi

Picha za wananchi wa Rulenge, Ngara wakimsikiliza na kumshangilia Mgombea Urais CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia leo.
Picha na Press Kikwete 2010











Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhiwa silaha za jadi na wananchi wa Rulenga ili aweze kujiandaaa vizuri cha uchaguzi.

Silaha hizo ni shoka la kufyekea visiki njiani anapopita kusaka kura za wananchi, panga kujilinda na hatari zilizombele yake na kusafisha njia na mwisho ni mkuki ambao ni ishara ya ushindi na uongozi. Wana Rulenga wameahidi kumpa kura zao zote za ndio Mgombea wa CCM Mheshimiwa Kikwete na wanaimanii atashinda kama kiongozi wa nchii na hivyo wamempa silaha hizo kama kiongozi.
Rulenga ambayo iko ndani ya Wilaya ya Ngara ni kituo cha pili baada ya Ngara Mjini ambapo msafara wa Mgombea Urais CCM ambapo kulikuwa na wananchi wengi na vikundi mbalimbali vya ngoma vikimsubiri.

Kabla ya kuanza hotuba yake, Mheshimiwa Kikwete alikosha nyoyo za wana Rulenga kwa kucheza wimbo wa pipi remix CCM Version ya mwanamziki wa kizazi kipya Marlow. Staili hii ya mgombea imekonga nyoyo za wana ccm wengi kote alikopita kwa staili yake ya uchezaji ambapo kundi la Vijana Zaidi wameipa staili hiyo jina la JK shafo (shuffle)
Baada ya Rulenga Mheshimiwa Kikwete alisimama Lusahunga kusalimia wananchi na baadae alielekea Biharamulo kwenye Mkutano wake wa tatu wa Kampeni kwa siku ya leo.

1 comment: