8/27/2010

Mkutano wa Kampeni Kigoma Mjini: JK-Tutajenga Uwanja wa Ndege Mpya Kigoma

PIUS NTIGA
27-8-2010
KIGOMA,
Mgombe Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete amewahakikishia wananchi wa Kigoma kuwa ujenzi wa uwanja wa Ndege Kimataifa wa kigoma utaanza rasmi kujengwa octoba mwaka huu.
Akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa mji wa kigoma na wana-ccm kwa ujumla katika uwanja wa lake Tanganyika amesema ujenzi huo utaenda sambamba na uwekaji wa njia mpya ya kurukia na sehemu ya kusubiria abiria.
Katika mkutano huo amesisisitza kuwa lengo la kuupanua uwanja huo ni kuchochea kasi ya maendeleo katika mkoa huo na kuinua kipato cha wananchi kupitia uwanja huu mkubwa wa kimataifa.
Mbali na hilo ametangaza kuwa hospitali ya mishipa ya fahamu itajengwa ndani ya Hospitali ya Muhimbili jijini Dare s salaam ambayo itakuwa kubwa katika nchi za Jjangwa la Sahara.
Pia mgombea huyo wa Urais kupitia CCM amewaambia wananchi wa Kigoma kuwa serikli imeipandisha hadhi Hospitali ya Maweni ya Mjini Kigoma kuwa hospitali ya rufaa huku akisisitiza kuwa hospitali nyingine ya wilaya ya Kigoma mjini itajengwa ili kupunguza msongamano katika hospitali hiyo ya rufaa.
Katika hatua nyingine amesema kwamba Oktoba mwaka huu serikali itaweka jiwe la msingi katika daraja la Mto Maragalas lengo likiwa ni kuwaondolea kero wananchi wa mkoa wa kigoma na vitongoji vyake.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi katika mkutano huo amesema hakuna mkoa unaobaguliwa kama inavyodaiwa hivyo akasisisitza kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuziletea maendeleo ya haraka mikoa hiyo inayodhaniwa kuachwa nyuma ikiwa ni pamoja na kigoma, kagera,lindi na mtwara.
Katika hatua nyingine mgombea ubunge wa jimbo la kigoma mjini PETER SERUKAMBA amewaomba wananchi wa Kigoma kutofanya tena makosa ambayo yalipelekea Halmashauri ya Mji wa Kigoma kuwa ya mchanganyiko wa vyama vya Chadema na CCM.
Kulingana na hali hiyo amewaomba uchaguzi huu kuwachagua wagombea wa udiwani wa CCM wote ili halmashauri huiyo iongozwe na CCM.

No comments:

Post a Comment