8/26/2010

Mkutano wa Kampeni – Ngara Mjini: CCM Inaaminika, Tujivunie Mafanikio Yetu

Mkazi wa Ngara mjini na watoto mapacha wawili akiwa amewahi na kupata sehemu ya kukaa kumsubiri mgombea wa Urais CCM, Mheshimiwa Kikwete alipohutubia wananchi wa Ngara leo katika uwanja wa Posta.
Mtoto wa Ngara akicheza ngoma kwa umahiri mkubwa kabla ya kusalimiana na Mgombea wa Urais wa CCM, Mheshimiwa Kikwete. Kabla ya kuanza hutuba yake ya kuomba kura, Mheshimiwa Kikwete alimpongeza mtoto huyu kwa kuenzi na kuendeleza tamaduni za kitanzania.Kampeni za Mgombea wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zimeingia siku yake ya sita ambapo zimeanzia na Mkutano wa Kampeni Wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.
Akisalimia umati mkubwa wa watu uliokusanyika kwenye Uwanja wa Posta Ngara Mheshimiwa Kikwete aliwaambia wana CCM wana kila sababu ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Alifafanua sababu mbalimbali zilizomsukuma yeye na Chama Cha Mapinduzi kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza nchi tena kwa mara ya pili. Mojawapo ya sababu hizo alizungumzia ni amani na utulivu uliopo nchini kwa sasa. Alisema hii inatokana na sera madhubuti za CCM zisizo na ubaguzi wa kabila, dini au mrengo wa siasa.
Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana Wilayani Ngara peke yake kwenye upande wa elimu ya msing/sekondari, Mheshimiwa Kikwete alieleza kwamba mwaka 2005 watoto 480 walichaguliwa kuingia kidato cha kwanza, na mwaka 2009 watoto 3840 wameingia kidato cha kwanza. Hii ni kutokana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2005 ya kujenga shule zasekondari kwa kila kata kwa kusaidiana na wananchi wa kata hizo.
Mafanikio mengine aliyazungumzia ni ya kwenye sekta ya afya, maji, kilimo na miundombinu ikiwemo jitihada za usambazaji wa umeme na maji pamoja na ujenzi wa barabara. Mwisho kabisa Mhishimiwa Kikwete alimnadi mgombea udiwani wa Ngara Mjini Charles Lujuba pamoja na madiwani wenzake wote wa CCM. Pia alimnadi mbunge wa CCM wa Ngara Deogratius Ntukamazina.
Kutoka Ngara mjini, msafara wa Mgombea Urais CCM ulisimama Ofisi za CCM Ngara na baadae kuelekea Rulenge.

No comments:

Post a Comment