8/23/2010

Mkutano wa Kampeni Buchosa Mwanza: JK "Tuliahidi, Tumetekeleza"


Mamia ya wananchi wa kijiji cha Nyehunge katika jimbo la Buchosa waliojitokeza kumsikiiza rais Jakaya Kikwete alipowatembelea na kuomba wampigie kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi leo amewaambia wakazi wa Buchosa kuwa CCM ni chama makini ilitoa ahadi mwaka 2005 na sasa wametekeleza.

 
Baadhi ya mafanikio yaliyofafanuliwa na Mheshimiwa Kikwete ni kama ujenzi wa shule za sekondari za kata ambapo sasa Buchosa ina shule nyingi zaidi ya kata zilizopo.

Aidha Mheshimiwa Kikwete pia alifafanua uendelezaji wa miundombinu ya Buchosa kama vile ujenzi wa barabara na usambazaji na upatikanaji wa umeme na maji safi.

Mheshimiwa Kikwete pia alichukua nafasi hiyo kuwanadi madiwani na mbunge wa Buchosa Dr, Tchizeni. Kabla ya kumkaribisha jukwaani hapo, Mheshimiwa Kikwete alimkaribisha Erick Shigongo ambaye alishindwa kwenye kura za maoni.

Baada ya Buchosa, Mheshimiwa Kikwete na msafara wake ulielekea Sengerema.

No comments:

Post a Comment