8/23/2010

Tuliahidi, Tumetekeleza - Sengerema, Sengerema

Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko kwenye kampeni zake za kutetea kiti cha urais kupitia CCM amewaambia wana Sengerema leo kwamba waichague tena CCM na viongozi wake kwani ni Chama kinachoaminika.
Rais Kikwete pia ameeleza safari zake nyingi za nje zimefanikiwa sana katika kuleta maendeleo nchini. Aliitolea mfano safari ya Marekani iliyojenga urafiki na ushirikiano na Rais George W. Bush ambaye amemuamini kiasi cha kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 700. Kutokana na msaada huo, Rais alisema ndio maana watu wa Sengerema watapata umeme siku za karibuni.
Rais Kikwete akiwa na furaha na hamasa tele, aliwaambia wana Sengerema kwamba yeye na serikali yake wamejipanga vizuri ili kuhakikisha kwamba yale yote waliyoyaanza 2005 yanaendelea 2010. Hivyo akichaguliwa tena na serikali yake, yale maendeleo yote yatafika Sengerema na kwa wa Tanzania wote kwa ujumla.
Aliongeza ya kuwa alipopita hapa mwaka 2005 alitoa ahadi kadhaa kwa kupitia ilani ya chama chake cha Mapinduzi. Naye kwa kupitia serikali yake ametimiza ahadi hizo zote, na pia Mbunge wa Sengerema amesaidia kuelezea mafanikio mengine.
Rais Kikwete pia aliwashukuru kwa wananchi kwa kumchagua mbunge wao arudi tena bila kuwa na mpinzani jimboni hapo. Pia alichukua nafasi hiyo kuwatambulisha madiwani wote wa Sengerema kupitia CCM. Aliwasihi wananchi kuwachagua wote ili kuhakikisha CCM inapita kwa kishindo baada ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment