8/22/2010

Mwenyekiti wa CCM Taifa arindima Mwanza

Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasihi wakazi wa Misungwi leo wachague CCM kwa staili ya mafiga matatu.


Rais Kikwete pia alielezea sababu za Chama chake cha CCM kuomba ridhaa ya wananchi kukichagua kwa sababu kuu tano:
1. CCM imeahidi na kutekeleza ahadi zake katika miaka mitano iliyopita.
2. CCM imeendesha nchi kwa amani na utulivu, na CCM itaendelea kufanya hivyo kama wakipewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kinachiokuja.
3. CCM inaendelea kutekeleza ahadi ili kuhakikisha maisha bora yanapatikana kwa kila Mtanzania
4. CCM ni chama makani, imara na kinaendelea kukua kila siku. Kwa maneno yake mwenyewe, Mgombea Urais Kikwete alisema "CCM Chama Dume, dume lenyewe la mbegu, vyama vingine vyote ni vichanga sana vinaiga mambo mengi kutoka kwetu".

5. CCM ni Chama chenye uzoefu na kimeendesha serikali kwa muda mrefu. Hivyo wakipatiwa ridhaa tena wataendeleza yale mazuri yaliyofanywa nchini tangu uhuru hadi sasa.

Mwisho kabisa Mgombea Urais Jakaya Kikwete aliwaomba wananchi wa Mwanza na wale wa Misungwi kuchagua chama chake kwa nafasi za madiwani, wabunge na Rais

No comments:

Post a Comment