8/19/2010

Rais Kikwete na Dr. Bilal awashukuru wana CCM Dar es salaam baada ya kurudisha Fomu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wanachama wa CCM waliojitokeza kumpongeza kwa hatua ya kurejesha fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi leo na pia kukubaliwa kama Mgombea halali wa CCM katika uchaguzi ujao.


Mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Dkt Mohamed Gharib Bilal akiwashukuru wanachama wa CCM na wapenzi waliofika leo katika viwanja vya Ofisi Ndogo ya CCM jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuwapongeza kwa kukubaliwa na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kuwa wagombea kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi ujao.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba (kushoto) akiteta na Mwenyekiti wa CCM, Dkt Jakaya Kikwete leo nje ya Ofisi Ndogo za CCM jijini Dar es salaam mara baada kurejea kutoka Tume ya Uchaguzi alipokuwa amerudisha Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi Mkuu ujao.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwasikiliza wagombea wao wakati walipokuwa wakihutubia maelfu wa wanachama wao katika ofisi ndogo ya chama CCM Lumumba.

(Picha na Tiganya Vincent-Dar es salaam)

No comments:

Post a Comment