10/17/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo Dar es salaamMgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akipandisha bendera ya CCM muda mfupi baada ya kufungua shina la wakereketwa la Rashid Mfaume Kawawa eneo la Magomeni Mzimuni jijini Dar es Salaam leo.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akipandisha bendera ya CCM muda mfupi baada ya kufungua shina la wakereketwa la Rashid Mfaume Kawawa eneo la Magomeni Mzimuni jijini Dar es Salaam leo.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCm Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa shina la wakereketwa la Rashid Mfaume Kawawa Magomeni Mzimuni jijini Dar es Salaam jana.
  

Mgombea urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mheshimiwa A. Kinana Mwenyekiti wa kampeni za CCM Taifa na mlezi wa CCM; mara alipowasili Magomeni kufungua shina la CCM. 

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia maelfi ya wakazi wa eneo la Manzese wakati wa mkutano wa kampeni jana mchana.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano wa Kampeni uliohutubiwa na Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana

Vijana machachari wa Tip Top Connection wakifanya vitu vyao Kawe leo

Wazee wa kazi wa Sikinde Ngoma ya ukae wakisubiri zamu yao kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania (CCM) Mheshimiwa Kikwete leo jioni.


Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zinaanzia Magomeni Kata ya Mzimuni kuzindua Shina la Wakereketwa la Mzee Rashid Mfaume Kawawa.

Kutoka Magomeni msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Manzese kwenye uwanja wa Bakhresa kwa mkutano mkubwa wa kampeni.

Mheshimiwa Kikwete pia atafungua shina la Wakereketwa la Waendesha pikipiki wa Mbezi Tanki Bovu na baada ya hapo kufanya mkutano wa kampeni Kawe viwanja vya Tanganyika Packers Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment