10/26/2010

Mkuto wa Kampeni Nkome:JK apokelewa kwa Kishindo

- Maelfu wajitokeza kumlaki kwenye mkutano wa kampeni
-Amnadi Mgombea Ubunge Bwana Donald Max na Madiwani wote wa CCM


Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Bugando alipowasili kwenye mkutano wa kampeni Nkome Wilayani Geita leo.

Maelfu ya wananchi wa Nkome wakimshangilia mgombea urais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anahutubia mkutano mkubwa wa kampeni leo Nkome.

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi Nkome leo

Mapokezi ya aina yake yamefanyika hapa Nkome Tarafa ya Bugando wilayani Geita Mkoa wa Mwanza kumpokea Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi.

Mheshimiwa Kikwete amefanya mkutano mkubwa wa kampeni kata hiyo akinadi sera za chama chake akisisitiza mipango madhubuti ya CCM kwa miaka mitano ijayo ikiwemo ujenzi wa barabara na uimarishaji wa huduma za afya na maji.

Kabla ya hapo Mheshimiwa Kikwete pia alisimama vijiji vya Kasota na Nzera wilayani Geita ambapo pia alifanya mikutano ya kampeni na kunadi sera za CCM na kuwaombea kura wagombea udiwani na mgombea ubunge wa jimbo hilo.

Ikiwa ni siku yake ya mwisho ya kampeni mikoani, Mheshimiwa Kikwete anategemewa kufanya mikutano ya kampeni Muganza, Chato (Kagera), Nyang'wale na hatimaye Mwanza mjini kwenye uwanja wa Nyamagana.

No comments:

Post a Comment