10/17/2010

Mkutano wa Kampeni Kawe: Tumefanikisha malengo kwa sababu tulithubutu kuanza - JK



Mheshimiwa Kikwete akielezea mpango wa serikali ya CCM wa kujenga barabara za juu maarufu kama "Fly-overs" jijini Dar es salaam kupunguza msongamano

Mheshimiwa Kikwete akielezea mpango wa serikali ya CCM wa kujenga barabara za juu maarufu kama "Fly-overs" jijini Dar es salaam kupunguza msongamano

Mheshimiwa Kikwete akimnadi Mama Kizigha, mgombea ubunge wa CCM Jimbo la kawe wakati wa mkutano mkubwa jimboni hapo leo jioni.

Umati wa wana CCM na wananchi wa Jimbo la Kawe waliokusanyika viwanja vya Tanganyika Packers leo jioni kuhudhuria Mkutano wa kampeni wa Mheshimiwa Kikwete


Umati wa wana CCM na wananchi wa Jimbo la Kawe waliokusanyika viwanja vya Tanganyika Packers leo jioni kuhudhuria Mkutano wa kampeni wa Mheshimiwa Kikwete

Msanii wa Bongo Fleva Diamond akitumbuiza leo Kawe kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema leo Jimboni Kawe CCM imefanikisha malengo yake kwa kuwa na uthubutu wa kutenda mambo ambayo wengi walidhani hayatekelezeki.

Mheshimiwa Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam  ambako aliwaambia wananchi mafanikio ya CCM sio ya kubezwa kwani yanaonekana.

Akizungumzia mafanikio ya elimu, Mheshimiwa Kikwete alielezea mafanikio ya sekondari za kata ambazo mwaka 2005 alipotoa ahadi hiyo, wengi walibeza kwa kusema haitekelezeki. Matokeo ya ahadi hiyo ni kwamba sasa hivi Mkoa wa Dar es salaam unapeleka zaidi ya wanafunzi laki mbili shule za sekondari kulinganisha na elfu sitini miaka ya nyuma.
"Hii ni kwa sababu tulithubutu kuweka ahadi hiyo na tumeitekeleza. Nilipita Tanga kule Lushoto nikaelezwa kuna kata ina sekondari saba, na watoto wanatosheleza. Haya ni mafanikio" alisema Mheshimiwa Kikwete.

Kwenye upande wa afya, Mheshimiwa Kikwete alisema CCM imejipanga ili kila jimbo la uchaguzi mkoani Dar es salaam liwe na hospitali yake ambayo ndiyo itakuwa hospitali ya Wilaya. Hospitali za Mwananyamala na Ilala zitakuwa za rufaa na Muhimbili itakuwa kwa ajili ya magonjwa makubwa ambayo kwa sasa wagonjwa hulazimika kwenda nje.

Akizungumzia janga la UKIMWI, Mheshimiwa Kikwete alisema wananchi wa Dar es salaam wachukue tahadhari na wakatae kupata UKIMWI. Maambukizi sasa kwa mkoa wa Dar es salaam ni asilimia 9.3 juu ya wastani wa taifa ambao ni asilimia 5.6. Mheshimiwa Kikwete aliongeza kuwa wa wanaopewa dawa za kurefusha maisha sasa wanafikia 61,435. Aliwataka wananchi wa Dar es salaam wasikilizi mafundisho ya dini na wachague kutokupata UKIMWI kwani Tanzania bila UKIMWI inawezekana.

Akifafanua mpango wa CCM wa kuboresha miundombinu jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Kikwete alielezea mpango mkubwa wa kujenga barabara za juu "fly-overs" ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa magari haswa kwenye makutano ya barabara kubwa.

Mheshimiwa Kikwete leo amefanya mikutano yake ya kampeni mjini Dar es salaam majimbo ya kinondoni, ubungo na kawe, kabla ya kuendelea na kampeni hizo mkoani Pwani kesho.

No comments:

Post a Comment