Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohamed Dewji |
-Mo Dewji acheza kwa furaha;
-Ashangilia mafanikio ya CCM Singida Mjini;
-Awasihi wana Singida wamwage kura zote CCM
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Dewji, amemfagilia Mheshimiwa Kikwete kwa kuongoza nchi na CCM vizuri.
Alisema hayo alipokuwa anasoma mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka mitano iliyopita na kusema wananchi wa Singida wamenufaika na mengi hata wakati wa mtikisiko wa uchumi na upungufu wa chakula wananchi wa Singida Mjini walipata msaada kutoka serikalini.
Kwenye upande wa upatikanaji wa maji safi na salama, Mo Dewji alisema sasa maji safi yanapatikana kwa asilimia 85, ukilinganisha na miaka mitano iliyopita. Vilevile kwenye elimu, alisema sasa Singida Mjini ina shule za sekondari zaidi ya ishirini ukilinganisha na shule mbili tu miaka mitano iliypita.
Hata hivyo alisema changamoto iliyopo kwa upande wa elimu ni ujenzi wa shule za kidato cha tano na sita ili wanafunzi wengi zaidi walioweza kuingia sekondari, waweze kuendelea na elimu ya juu.
Changamoto nyingine ni upande wa afya na ugonjwa sugu wa macho (mtoto wa jicho), ambao alieleza unatokana na hali ya hewa ya mji wa Singida. Alieleza mgombea huyo kwamba amefanya jitihada kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali na hadi sasa wagonjwa mia tano wamefanyiwa upasuaji kati ya wagonjwa elfu mbili.
Mwishoni alimnukuu baba wa Taifa Mw. Julius Nyerere akiwasihi wana Singida wafanye maamuzi mazuri ya kuchagua viongozi bora kipindi cha uchanguzi. "Na viongozi bora wanapatikana ndani ya Chama Cha Mapinduzi, CCM Oyee, hivyo chagueni CCM iendelee kuongoza" Alimaliza mgombea huyo wa ubunge kijana.
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia umati mkubwa wa watu kwenye mkutano wa Kampeni Singida Mjini Leo tarehe 2.10.2010 |
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Singida Mjini Mohamed Dewji akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Jimbo la Singida Mjini kabla ya hotuba ya Mgombea Urais wa Chama hicho Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete tartehe 2.10.2010
No comments:
Post a Comment