10/17/2010

Mkutano wa Kampeni Manzese


Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais kupitia chama hicho Mheshimiwa Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo nndugu Hawa Ng'umbi kwa wananchi wa Manzese wakati wa mkutano wa kampeni tarehe 17.10.2010.


Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa Manzese wakatiwa mkutano wa kampeni tarehe 17.10.2010.

Umati mkubwa wa wananchi wa Manzese wakisikiliza hotuba ya kampeni kutoka kwa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete wakati akihutubia mkutano wa kampeni huko Manzese tarehe17.10.2010






Umati mkubwa wa wananchi wa Manzese wakisikiliza hotuba ya kampeni kutoka kwa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Kikwete wakati akihutubia mkutano wa kampeni huko Manzese tarehe17.10.2010
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameomba kura leo Manzese Jimbo la Ubungo Dar es salaam akisema CCM ni Chama kinachotimiza ahadi zake.

Akizungumzia ahadi zilizotekelezwa kwenye ilani ya CCM 2005-2010 kwenye uboreshaji wa huduma za jamii Mheshimiwa Kikwete alisema Dar es salaam ya leo si ile ya miaka 20 iliyopita.

Kwa upande wa elimu ya sekondari, miaka mitano iliyopita, Dar es salaam ilikuwa na shule za sekondari chini ya 25 na sasa kuna shule za sekondari zaidi ya 100. "Haya ni mafanikio makubwa mno kwenye sekta ya elimu ambayo yamekuja na changamoto zake za maendeleo tutazikabili" Alisema Mheshimiwa Kikwete.

Akizungumzia huduma ya afya na jitihada za CCM na serikali kupambana na magonjwa makubwa, Mheshimiwa Kikwete alizungumzia gonjwa la Ukimwi kwa kirefu. Alisema wananchi 61,433 mkoani Dar es salaam wanahudumiwa kwa kupewa dawa za kurefusha maisha Dar es salaam ikiwa ni mkoa wa tatu kwa maambukizi ya UKIMWI asilimia 9, ikiwa na maana kwa kila watu 100, tisa wameathirika na maradhi ya UKIMWI.

Kwenye mpango wa kuendeleza wananchi kiuchumi, Mhehshimiwa Kikwete alisema itajengwa machinga complex mbili, ambapo wafanyabiashara wadogowadogo zaidi ya elfu arobaini watapata nafasi ya kufanya bishara zao.

Pia alisema jengo kubwa la viwanda litajengwa ambapo wanyabiashara hao watapata nafasi ya kuzalisha bidhaa zao wenyewe na kuziweka sokoni.

"Hawa ni watu wengi sana ndugu zangu, tuzingatie mafundisho ya dini na tukatae kupata UKIMWI" Alimalizia Mheshimiwa Kikwete kwenye afya.

Mwisho alimnadi Mgombea udiwani wa Jimbo la Ubungo, Mama Hawa Ngumbi ambaye alisema wana Manzese wawape CCM ushindi wa utatu, kama matairi ya bajaji ambapo kama moja likitoka bajaji haitembei.

No comments:

Post a Comment