10/06/2010

Mapokezi ya kishindo yamsubiri JK Uwanja wa Demokrasia Kipandamaiti


Barnaba, CCM Oyee

Barnaba na Lina, wrong number

Marlow akiimba CCM Pipi "Tumeanza kupiga honi na Pipi, Haooo Hawaelewani" uwanja wa demokrasia leo jioni

Marlow "Kiduku" style

Umati wa wana CCM na wananchi wa Unguja waliofurika uwanja wa demokrasia kipandamaiti

Utenzi


Kikundi cha Taarab cha Big Star kikitoa burudani

Maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni Unguja

Mwanachama wa CCM akiimba wimbo wa Marlow wa pipi wakati mwanamziki huyo alipoingia jukwaani kutumbuiza


Kikundi cha kiduku kutoka Dar es salaam kikitoa burudani kwa staili ya pekee


Wana CCM wakicheza kwa pamoja kabla ya mkutano wa kampeni kuanza

Msafara wa Mheshimiwa Kikwete unasubiriwa kwa nderemo na vifijo sasa hivi hapa kwenye uwanja wa Demokrasia Kipandamaiti Unguja.

Vikundi mbalimbali vya burudani vimeshapanda jukwaani kutoa hamasa kabla ya mkutano wa kampeni kuanza.

Kikundi maarufu cha taarab cha BigStar cha Mkoa Mkuu Magharibi hapa Unguja kilirusha roho za wana CCM na wananchi waliofurika kwa maelfu kuhudhuria mkutano wa kampeni wa Mheshimiwa Kikwete.

Burudani nyingine zilizotumbuiza ni Barnaba na Lina kutoka Dar es salaam, Marlow, Mheshimiwa Temba na Chege, Diamond wote wakiwa na nyimbo zao mpya za uchaguzi na CCM.

Za Origino Komedi nao hawakuwa nyuma, walionekana uwanjani na kuvutia umati mkubwa wa watu kabla hata ya kupanda jukwaani.

Baada ya kupanda jukwaani, ze komedi waliwapagaisha wananchi waliofurika kwa burudani waliyoitoa na misemo ya "usichague wapinzani baba hapendi".

Mheshimiwa Kikwete na msafara wake umewasili leo mchana ukitokea Pemba baada ya kufanya mkutano mkubwa wa kampeni Chakechake jana jioni. Leo anatarajiwa kupanda jukwaani saa kumi na moja jioni baada ya burudani zinazoendelea sasa.

No comments:

Post a Comment