Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Karatu na vitongoji vyake wamefurika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo jioni hii.
Mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Karatu mjini ulifurika wana CCM na wananchi waliokuwa na hamasa kubwa ya kumsikiliza Mheshimiwa Kikwete.
Umati huo kwa ujumla wake ulimueleza Mheshimiwa Kikwete kwamba wananchi wa Karatu wamechoshwa na sera za upinzani ambazo zimeshindwa kuleta maendeleo kwa miaka mingi.
Akiwauliza wananchi hao iwapo wako tayari kuipigia kura CCM na madiwani wake na mbunge, wananchi wao kwa ujumla wao wote walinyanyua mikono na kuonyesha ishara ya kuikubali CCM na kuwa wataipa kura zote.
Mkutano huo uliochangamka na uliokuwa na shamrashamra nyingi, ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumai ambaye aliwasalimu wananchi na kuwaomba wachague CCm kwa maendeleo ya kweli.
Mkutano huu ni wa mwisho kwa siku ya leo ambapo Mheshimiwa Kikwete alianzia Kibaya na Matui Mkoani Manyara.
Baada ya Matui, msafara wa Mheshimiwa Kikwete ulielekea Olkesumet na Mang'ola, kabla ya kuingia hapa Karatu mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment