10/01/2010

Mkutano wa Kampeni Rostam waitikisa Igunga

Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Igunga Mkoani Tabora Rostam Aziz

Umati wa watu wakifuatilia mkutano wa kampeni Igunga Tabora leo

Vuvuzela Igunga

NaTamali Vullu, Igunga

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amesema angeshangaa iwapo mgombea ubunge wa jimbo la Igunga, Rostam Aziz, angekuwa na mpinzani kutokana na maendeleo yaliyofanya jimboni humo.

Kikwete alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Sabasaba ulioko mjini Igunga, Mkoa wa Tabora wakati akimwombea kura mgombea huyo.

"Rostam mmemuona… namuombea kura, ninyi mnamjua zaidi kuliko mimi, ameeleza mwenyewe aliyoyafanya, ningeshangaa kama angekuwa na mpinzani. Kama ni timu ya mpira, Rostam amekamilika idara zote kuanzia ulinzi, ushambuliaji na katikati, mpate nini jamani kama Rostam Azizi,"alisema Rais Kikwete.

Alisema Rostam amefanikiwa kuibadilisha wilaya hiyo kwa kuwa miaka ya nyuma ilikuwa nyuma kimaendeleo, lakini sasa inaonekana mji unaoheshimika.

"Mwaka 1980 hadi mwaka 1983 nilikuwa Katibu Mtendaji wa CCM, Mkoa wa Tabora, Igunga naifahamu kwa sababu nilikuwa nakuja, ilikuwa na nyumba za matope ambazo zinamong’onyoka, wakati huo Igunga kilikuwa kama Kijiji. Kwa sasa imebadilika, tatizo liliobaki ni barabara,” alisema.

Kikwete aliwaahidi wakzi hao kuwajengea kilomita tatu za barabara ya lami ili mji huo uwe na hadhi ya mji na pia watatekeleza ahadi za ujenzi wa barabara zilizotolewa na Rais Mstaafu, Benjamni Mkapa.

Aidha, aliwatoa hofu wakazi wa Jimbo hilo kuwa serikali yake ijayo italijenga daraja la Mbutu, ili kuwaondolea kero ya muda mrefu na kuongeza kuwa ujenzi wa daraja hilo ni muhimu ingawa unahitaji fedha nyingi kulikamilisha.

Kwa upande wake, Rostam alijivunia mafanikio aliyoyafanya jimboni humo kwa kusema kuwa, Igunga ya mwaka 1994 si ya sasa kwani amefanikiwa kuibailisha kwa kiasi kikubwa.

"Zamani Igunga ilikuwa ya mwisho kwa kila kitu katika Mkoa wa Tabora, ilikuwa ya mwisho katika sekta ya elimu, afya na nyinginezo, lakini sasa wilaya hii inaongoza katika Mkoa wa Tabora. Kwa mfano, mwaka 1995, wilaya ilikuwa na sekondari tatu lakini sasa zipo 32 na zahanati zilkuwa tisa, lakini sasa zipo 75.

"Pamoja na jitihada hizo, ndani ya miezi 12 ijayo kuanzia sasa, kila kijiji kitakuwa na zahanati yake. Pia katika sekta ya maji, vijiji 65 kati ya 96 vilivyoko wilayani hapa vinapata ya maji na pia tumechimba mabwawa 45,"alisema Rostam.

Alisema anaamini ndani ya mitano ijayo, tatizo la maji linalowakabili wananchi litakuwa limetatuliwa ipasavyo kutokana na jitihada za serikali ijayo ya CCM na kwa upanse wa umeme alisema vijiji 20 vinapata nishati hiyo.

No comments:

Post a Comment