10/30/2010

Mkutano wa Kampeni Jangwani, Dar es salaam
Baada ya siku 69 za kampeni kutetea kiti chake cha urais, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo anahitimisha kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es salaam.

Akitoa utangulizi kabla ya Mheshimiwa Kikwete kuhutubia maelfu ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM Lt. Mstaafu Yusuph Makamba alisema Mheshimiwa Kikwete amefanya kampeni safi iliyojumuisha mikutano 330 nchi nzima, na alisafiri kwa barabara na anga umbali wa kilometa 22,000 nchi nzima.

Mheshimiwa Kikwete anategemewa kuhutubia mkutano huu mkubwa muda mchache kutokea sasa, baada ya katibu wa chama kuongea na mgombea mwensa Dr. nilal Hutuba hiyo itarushwa moja kwa moja vituo vya Start TV na TBC na kwenye mtandao itarushwa moja kwa moja na VIZA TV kupitia habaricom.

No comments:

Post a Comment