10/03/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete leo

Msafara wa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo unamalizia kampeni zake Mkoani Singida na baadaye kuingia Dodoma.

Mkutano wa kwanza wa kampeni utafanyika kijiji cha Puma na baada ya hapo utaenda kijiji cha  Ikungi.ambapo pia kutafanyika mkutano  wa kampeni.

Baadaye mchana kutakuwa na mkutano wa kampeni Itigi, Manyoni na Kitinku, kabla ya kumalizia na mkutano mkubwa wa kampeni Dodoma Mjini.

No comments:

Post a Comment