10/03/2010

Mkutano wa Kampeni Manyoni: Chiligati ampongeza JK kuleta maji Manyoni


Mheshimiwa Jakaya  Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni Manyoni Mashariki leo tarehe 3.10.2010
 
Mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki John Chiligati akimmwagia sifa Mheshimiwa Kikwete na CCM wakati akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM jimboni hapo.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza kabla ya Mheshimiwa Kikwete kuwasili kwenye uwanja wa mkutano

Mheshimiwa Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa mkutano tayari kuhutubia wananchi wa Manyoni kwenye mkutano wa kampeni leo jioni.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Mheshimiwa John Chiligati amemmwagia sifa Mheshimiwa Kikwete kwa kutatua tatizo la maji Manyoni mjini. Alisema tnagu Mheshimiwa Kikwete aingie madarakani, ametembelea Manyoni mara nne na muda wote amekua akiahidi kutatua tatizo la maji.

Aliongeza ya kwamba visima na gharama za kusambaza maji zilikuwa juu mno na Mheshimiwa Kikwete aliahidi kugharamia nusu ya gharama hizo kiasi cha shilingi milioni 300, ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Chiligati aliyasema hayo alipokuwa akielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa kampeni Manyoni Mjini leo.

Kwa upande wa elimu Chiligati alisema kuwa kwa sasa Manyoni ina shule za sekondari 11 ukilinganisha na shule nne tu miaka mitano iliyopita. Aliongeza kuwa sasa lugha ya kusema watoto wanaomaliza darasa la saba wanachaguliwa kuingia sekondari sasa imeisha. "Sasa kila mtoto anayefaulu mtihani wa darasa la saba anaendelea na masomo ya juu" Alisema Chiligati akishangiliwa na maelfu ya wakazi wa Manyoni.

Sifa hizo hazikuishia kwenye elimu tu pia alizungumzia ujenzi wa Barabara ya Manyoni - Singida ambayo alisema zimebaki kilometa chache sana hadi kumalizika. Pia alizungumzia mafanikio kwenye upande wa afya, maendeleo ya mifugo na kilimo na hatimaye mpango wa kurasimisha mali za wanyonge MKURABITA. Kwenye hili alisema vijiji vimeshaanza kupimwa ili kukamilisha zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment