10/02/2010

Mkutano wa Kampeni Nduguti, Wilayani Iramba - Singida: JK apokelea na vikundi vya kwaya na nyimbo za kumsifu

Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na kiongozi wa kikundi cha kwaya cha kata ya Iguguno leo mara baada ya kikundi hicho kutumbuiza katika mkutano wa kampeni Nduguti, Singida.
Vikundi vya kwaya vya Nduguti vimesihi wana Singida na watanzania kwa ujumla kumchagua Mheshimiwa Kikwete na CCM kwani kufanya vinginevyo ni kupoteza muda.

Vikundi hivyo kutoka kata za Ilunda na Iguguno  vilisisimua umati wa watu uliohudhuria mkutano huo kwa maneno ya hamasa na mshikamo, vilielezea mafanikio ya serikali ya CCM na maendeleo yaliyoletwa na Mheshimiwa Kikwete kwa kipindi chake cha uongozi miaka mitano iliyopita.

Akisoma mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya CCM 2005 - 2010, katibu wa CCM wilaya alielezea mafanikio kwa upande wa elimu, miundombinu, vituo vya afya na upatikanaji wa maji safi.

Kabla ya kusimama Nduguti, msafara wa Mheshimiwa Kikwete uliotokea Kiomboi Iramba ulisimama vijiji vya Ulemba, Kiele, Kinampanda, Msingi na Bimanga Wilayani Iramba. Baadaye mchana huu wa leo, msafara huo unatarajiwa kuingia Singida vijijini na baadae Singida mjini kwa mkutano wa mwisho wa kampeni.

No comments:

Post a Comment