Mgombea urais wa CCM Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi mgombea ubunge Jimbo ls Igunga Rostam Aziz katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga mchana huu
Mshairi Mwana Igunga akighani leo
Mwanaigunga akipongezwa na Mh Jakaya Mrisho Kikwete
Mheshimiwa Rostam Azizi akihutubia umati uwanja wa SabaSaba Igunga leo
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wana Igunga leo
- Mapokezi mazito kwa JK- Waahidi kura za CCM 100%
- Wawasihi majimbo jirani kutochagua upinzani
- Rostam asisitiza Igunga ya 2010 si ile ya 1995
- Rostam asisitiza Igunga ya 2010 si ile ya 1995
Kwenye msafara wa Mamba kenge hawakosekani!
Ndivyo shairi la mwakilishi wa watu wa Igunga lilivyosema kuwaasa wananchi wawe makini wakati wa kupiga kura. Msoma shairi aliyejitambulisha kama Ali Nkindwa, mwenye asili ya kinyaturu, alisema wapinzani hawana nafasi Igunga wala Tanzania kwa ujumla kwani bado wako kwenye majaribio.
Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Igunga, Mheshimiwa Rostam Aziz, alisema Igunga ya 1995 si sawa na Igunga ya sasa mwaka 2010. Kwenye upande wa afya, igunga sasa ina zahanati 74 ukifananisha na zahanati tisa tu 1995.
Aliongeza kuwa Igunga ni wilaya kame sana, na kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, CCM imejitahidi kutatua tatizo la maji kwa kiasi kikubwa. Sasa vijiji 64 vinapata maji ya uhakika sasa. Alimuomba Mheshimiwa Kikwete kutupia macho tena kwenye jimbo hilo ili kuhakikisha tatizo hilo linakwisha kabisa.
Kwa upande wa umeme vijijji 21 vina umeme ambapo imefanya Igunga kuwa wilaya ya kwanza mkoani Tabora kwa kuwa na vijiji vingi zaidi vyenye umeme.
Kwa upande wa elimu, Mheshimiwa Rostam Aziz alisema sasa Igunga ina shule za kata 32 na hali Wilaya ya Igunga ina kata 26 tu. Ina maana ya kwamba ziko kata ambazo kuna shule zaidi ya moja.
"Haya ni mafanikio makubwa na ni kwa sababu ya CCM, Igunga sasa imebadilika" alimaliza mgombea huyo wa ubunge ambaye amekuwa Mbunge kwenye Jimbo la Igunga tangu mwaka 1995.
No comments:
Post a Comment