10/30/2010

Mkutano wa Kampeni Jangwani - Mzee Ruksa na Mkapa wampigia chapuo JK

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa akimpongeza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Wakati mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Kikwete ukiendelea viwanja vya Jangwani, marais wastaafu wa awamu ya pili na ya tatu wamemnadi Mheshimiwa Kikwete leo.

Akimnadi Mheshimiwa Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa amewasuta waliosema amemtelekeza Rais Kikwete na kampeni zake. Alisema kamwe hawezi kumuacha Rais Kikwete kwani uongozi wake unasifika dunia nzima.

Mheshimiwa Mkapa alisema amemjua Rais Kikwete na kufanya naye kazi muda mrefu tangu akiwa mkuu wa wilaya yake. Walifanya kazi kwa pamoja kuukimbiza mwenge na kuukabidhi wilaya inayofuata.

Mheshimiwa Mkapa alisema anatambua kuwa Rais Kikwete ana dhamira ya kuongoza, anaijua hali halisi ya nchi yetu kisiasa, kiuchumi na kwa kila hali. Hakuna mgombea kama yeye. "Wagombea wengine wanaitana mmoja ni Kilimanjaro mwingine ni kichuguu. Mimi nasema wote ni kokoto!"

 
Umati wa wanachama wa CCM katika viwanja vya jangwani waliohudhuria mkutano wa kilele cha kampeni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Umati wa wanachama wa CCM katika viwanja vya jangwani waliohudhuria mkutano wa kilele cha kampeni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Umati wa wanachama wa CCM katika viwanja vya jangwani waliohudhuria mkutano wa kilele cha kampeni jijini Dar es Salaam leo mchana.
Alisema anasikitika kuwa hakupata nafasi ya kwenda Zanzibar kuwasihi waendeleze amani na utulivu wakati wa uchaguzi. Alisisitiza kuwa anaunga mkono uamuzi wa wazanzibari wa kuunda serikali ya muungano, lakini anaamini kuwa ni CCM pekee ndiyo itakayoweza kuongoza na kuendeleza mapinduzi ya 1964.

No comments:

Post a Comment