9/04/2010

Jamhuri Stadium Yafurika - Mkutano wa Kampeni Morogoro Mjini

Pikipiki ikiongoza kumsindikiza Mgombea wa CCM Mheshimiwa Kikwete wakati msafara wake ukiingia Morogoro mjini.
Mgombea Urais wa CCM Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa CCM Morogoro mjini Aboud kwenye uwanja wa Jamhuri leo.

Mheshimiwa Kikwete akihutubia umati wa watu uliofika Jamhuri Stadium jioni ya leo kuhudhuria Mkutano wa kampeni.
Uwanja wa Jamhuri ulioko mjini hapa jioni hii umefurika umati na mashabiki wa CCM waliofika kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aki inadi chama chake cha CCM.

Mkutano huo ulipambwa na maandamano ya magari na pikipiki pamoja na vikundi vya sanaa na burudani.

Wa kwanza kupanda kwenye jukwaa la wasanii alikuwa Juma Nature na kundi lake, na baadae Bushoke ambaye naye pia aliburudisha umati huo kwa kubadili maneno ya wimbo wake maarufu wa "linawachoma kumpenda JK na kuona barabara zimejengwa kwneye kiwango cha lami." Baada ya Bushoke aliimba Marlow na wimbo wake wa pipi CCM remix.

Msanii wa Morogoro aliwatumbuiza wengi pale alipoigiza sauti za viongozi mbalimbali ikiwemo sauti ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na yake mwenyewe Mheshimiwa Kikwete.

No comments:

Post a Comment