9/05/2010

Ratiba ya Kampeni ya Mheshimiwa Kikwete Leo

Msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaanzia Wilayani Kilosa kwa siku ya leo kutokea Morogoro mjini. Msafara huo utasimama Kimamba kabla ya kuingia Kilosa Mjini.

Kutokea Kilosa, msafara wa Mgombea Urais kupitia CCM Mheshimiwa Jakaya Kikwete utaelekea Dumila na Mvomero ambapo mheshimiwa atasimama kusalimiana na wananchi wa maeneo hayo.

Baadae msafara utaishia Turiani kwa Mkutano wa Kampeni ambapo Mheshimiwa Kikwete anategemewa kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chake cha kwanza na mengine anayotazamia kuyafanya akipata ridhaa ya uongozi.

No comments:

Post a Comment