9/22/2010

Mkutano wa Kampeni Ifunda - JK awasihi watanzania kuepuka siasa za ubaguzi

Kampeni za Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasihi wananchi wa Ifunda, Kalenga Iringa kuwa waepuke siasa za kibaguzi ili kuekwepa machafuko ya nchi haswa kipindi cha uchaguzi.

"Wakija na sera zao za kibaguzi wakatalieni, waambieni tuambieni sera zenu za kisiasa sio za kibaguzi, hizo zikataeni"

Alisema serikali ya CCM inakusudia kulinda usalama wa wananchi na Watanzania kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi yetu.


Akinadi sera za CCM, Mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Mheshimiwa Kikwete alisema kwa upande wa elimu, CCM imeshika hatamu kwenye kuhakikisha changamoto za elimu zinakabiliwa sawasawa kwa miaka mitano ijayo.

Mheshimiwa Kikwete pia alichukua nafasi kwenye mkutano huo kumnadi Dr. Mgimwa, mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga. Alieleza kuwa Dr. Mgimwa ni muadilifu na mvumilivu sana, kwani hii ni mara yake ya tatu kuomba ridhaa ya wananchi kuongoza jimbo hilo. Alisema Dr. Mgimwa ana uzuefu kwenye uongozi, anayo ari kubwa na mawazo mengi ya kuongoza Jimbo la Kalenga. "Mimi namuamini na wenzangu ndani ya CCM tunamuamini hivyo naomba nanyi wananchi mumuamini na kumpa kura nyingi mwezi ujao"

Kutoka Ifunda msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Mufindi kwa mkutano wa kampeni.

No comments:

Post a Comment