9/18/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo atafanya mikutano ya kampeni Wilaya za Mbulu, Hanang na Babati.
Mkutano wa Kwanza wa kampeni utafanyika Kata ya Dongobesh wilayani Mbulu ambapo Mheshimiwa Kikwete jana amemalizia kwa mkutano mkubwa wa kampeni.
Baadaye msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Hydom wilayani Mbulu.
Kutokea Hydom msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaendelea Wilaya ya Hanang; Basotu, Katesh na Endasaki.
Mheshimiwa Kikwete atamalizia mikutano yake ya kampeni kwa siku ya leo Wilayani Babati ambapo atafanya mikutano ya kampeni Dareda na Babati Mjini.

No comments:

Post a Comment