9/15/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo Kilimanjaro

Mkutano wa kwanza wa kampeni za mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa siku ya leo utafanyika Tarakea , Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Baadae msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Himo mkoani humu kwa barabara kupitia Mkuu Rombo, Mengwe na Mwika ambapo Mheshimiwa Kikwete atafanya mikutano ya kampeni kwenye maeneo yote hayo.
Kutokea Himo, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Marangu Mtoni, Kirua Vunjo, Kawawa Road na baadae kuingia Moshi Mjini. Mheshimiwa Kikwete atafanya mikutano ya kampeni vituo vyote hivyo na mwisho atakuwa Uwanja wa Mashujaa Moshi Mjini.

No comments:

Post a Comment