9/19/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo Manyara - Kondoa

Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zitaanzia Galapo, ambapo ni kituo cha mwisho kwa Mkoa wa Manyara.
Kutokea Galapo, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Kondoa kwa kupitia vituo Hului, Madisa, Atta, Mkandulu na Bumbuta ambapo atahutubia wakazi wa maeneo hayo.
Baada ya vituo hivyo, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Mrijo na Mondo ambapo Mheshimiwa Kikwete atafanya mikutano ya kampeni maeneo hayo.
Kituo cha mwisho cha kampeni kitakuwa Kondoa mjini ambapo atafanya mkutano mkubwa wa kampeni Kondoa Mjini.

No comments:

Post a Comment