9/19/2010

Mkutano wa Kampeni Kondoa Mjini jioni hii

Mheshimiwa Kikwete akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kondoa, Mheshimiwa Zubein Mhita baada ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni Kondo Mjini leo hii.

Maelfu ya wanachama wa CCM wamempa mapokezi makubwa Mwenyekiti wa CCM taifa na mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Kondoa mjini alipowasili kufanya mkutano wa kampeni.


Mheshimiwa Kikwete alichukua muda mwingi wa hotuba yake kufafanua jitihada zitakazochukuliwa na CCM kama ikirudi kuongoza serikali kuhakikisha kuwa huduma bora ya afya inapatikana kwa kila Mtanzania. Alielezea ujenzi wa zahanati kila kata, utoaji wa vyandarua viwili kwa kila kaya, na jitihada za kuchanja wanawake bure kuzuia kansa ya shingo ya uzazi.


Kwa upande wa utoaji huduma ya maji, Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa vijiji 27 vya Kondoa Mjini vitapata maji ya uhakika kwa kupitia mpango mkubwa wa kusambaza maji kwa kushirikiana na Benki ya dunia. Mheshimiwa Kikwete alisema wilaya nyingi nchini mpango huu unashirikisha vijiji 10 hadi 15, lakini kwa kutambua ukubwa wa tatizo la maji Wilayani Kondoa ndipo maamuzi ya vijiji 27 yalifikiwa.


Mheshimiwa Kikwete pia alifafanua mafanikio yaliyopatikana kwenye upande wa elimu ya msingi na sekondari, sekta ya kilimo na mifugo, uwezeshwaji wa wananchi kiuchumi na ujenzi wa barabara.


Mwishoni Mheshimiwa Kikwete aliwanadi wagombea udiwani na ubunge na kuomba wananchi wachague CCM na wagombea wote kwa staili ya mafiga matatu.

No comments:

Post a Comment