9/14/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo

Kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo zinaanzia Lushoto mjini kwa mkutano mkubwa wa kampeni.
Baada ya Lushoto mjini, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Mombo, Tanga kwa ajili ya mkutano mwingine wa kampeni.
Kutoka Mombo, Mheshimiwa Kikwete atafanya mkutano wa kampeni Ndungu wilaya ya Same Mashariki mkoa wa Kilimanjaro.
Vituo vingine vya kampeni kutokea Ndungu ni Maore ambapo atasimama na kufanya mkutano na wakazi wa maeneo hayo kabla hajafanya mkutano mkubwa wa kampeni Kisiwani na baadae Same.
Kutokea Same, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Mwanga ambapo ndio kituo cha mwisho kwa siku ya leo.

No comments:

Post a Comment