9/22/2010

Kampeni za Mheshimiwa Kikwete Leo

Kampeni za mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo ziko Mkoani Iringa na zitaaza kwa mkutano mkubwa wa kampeni Ifunda kupitia Tanangozi ambapo Mheshimiwa Kikwete atazungumza na wananchi wa hapo.
Baada ya Ifunda msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Mafinga na Igowole kwa barabara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kabla ya kuelekea Lupembe.
Mkutano wa mwisho wa kampeni kwa siku ya leo utakuwa Njombe Mjini, ambapo Mheshimiwa Kikwete atakuwa amemaliza siku mbili za mkutano Mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment